THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

JK azindua ujenzi wa Jumba la mikutano na makao makuu ya CCM na kitega uchumi mjini dodoma leo

 Michoro ya majengo ya Ukumbi,Ofisi za Makao makuu na Hotel ya nyota tano vya CCM yalioanzwa kujengwa mjini Dodoma.
 Muonekano kwa mbali
 Mchoro wa jengo la hoteli ya nyota tano
 .Rais wa Zanzibar akiwasili eneo la Makulu mjini Dodoma kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za makao makuu ya CCM, Ukumbi wa Mikutano na Hotel ya Hadhi ya nyota tano leo.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Chama,Ukumbi wa Mikutano na Hotel za Hadhi ya Nyota Tano katika eneo la Makulu Dodoma leo


Kuna Maoni 8 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Nimekubali...Dom itapendeza

 2. Anonymous Anasema:

  Chama kina miradi gani ya kufadhili ujenzi huo, maelezo tafadhali.

 3. Anonymous Anasema:

  Chinese wanatununua sasa..

 4. Anonymous Anasema:

  ufisadi tu. raia hawa afford matibabu, hamna madawa mahospitalini. miradi gani isiyoinufaisha taifa.

 5. Anonymous Anasema:

  Mwanzo mlijenga Chamwino kwa kodi za wananchi!
  Mkajenga tena Chimwaga kwa kodi za wananchi!
  Sasa tena mnajenga ukumbi mwingine kwa kupata pesa toka wapi?
  Viwanja vya mpira vyote mmejimilikisha! Wakati mlikuwa mkipita nyumba hadi nyumba kuchangia kwa lazima wakati wa ujenzi wa viwanja vile! Nakumbuka nilikuwa na duka langu la jumla wakati ule nililazimishwa kutoa pesa nyingi sana ili kuchangia ujenzi wa viwanja hivyo!
  Virudisheni kwa wananchi vyote ili pato la taifa liingie sio kuota viwanja vya ccm.
  Naomba wabunge muulize ccm ina miradi gani mikubwa ya kuweza kujenga ukumbi mkubwa wa mikutana na hotel ya nyota tano, kama sio ufisadi na mahesabu ya pesa za wananchi wanachukua bila wananchi kujua?
  Najua Michuzi, hii huwezi kuitoa kwa sababu na we unaingia polepole kwenye kundi hilo!

 6. Anonymous Anasema:

  Kwa nini CCM iswe na majengo mapya? Si majengo tu. CCM ime uza mji wa Dar ime wazulumu wananchi majumba kwa kuzia wageni.Hakuna kipya, Baada ya mkutano na sharehe yale yale ya zamani ndiyo yata rundi. Uchawai ume kwisha sasa.Tanzania itasonga mbele.

 7. Anonymous Anasema:

  kwa mtaji huu chadema kuingia ikulu ni ndoto mbaya sana

 8. Anonymous Anasema:

  Acha wajenge wakati wa Watanzania kuchukua mali zao ukifika haya yote yatakuwa mali ya umma tu. Kumbuka chama cha KANU kule Kenya walijimilikisha ukumbi wa Kenyatta International Conference Centre (KICC), lakini baada ya NARC kuingia madarakani walitaifisha kituo hicho mara moja. Suala sio CHADEMA, CUF wala TLP kuingia madarakani suala ni mali za umma kuwa mikononi mwa umma, na si kuwaachia majambazi wa CCM. Na muda huo unakaribia kwa kasi sana. Wazalendo iweni na matumaini ya Tanzania njema na yenye neema bila mzimu na ajenti wa ibilisi CCM.