NA MOHAMMED MHINA, ZANZIBAR

TUME YA RAIS WA ZANZIBAR YA KUCHUNGUZA CHANZO CHA AJALI YA MELI YA SKAGIT, LEO IMETOA RIPOTI YAKE KWA WAANDISHI WA HABARI NA KUBAINISHA BAADHI YA KASORO NA KUTOA MAPENDEKEZO YA HATUA ZA KUCHUKUA KWA WALE WOTE WALIOHUSIKAKATIKA AJALI HIYO.

AKITOA TAARIFA YA TUME KWA WAANDISHI WA HABARI MJINI ZANZIBAR, KATIBU MKUU KIONGOZI WA SMZ BW. ABDULLAHAMID YAHAYA MZEE, AMESEMA TUME IMEBAINI KUWA TAARIFA ZA IDADI YA ABIRIA WALIOPANDA MELI SIKU YA TUKIO ILIKUWA NI POTOFU.

AMESEMA TUME HIYO IMEBAINI PAMOJA NA MAMBO MENGINE, KUWA MELI HIYO ILIKUA NA IDADI YA ABIRIA 447 WAKIWEMO WATANZANIA 429 NA RAIA WA KIGENI 18 TOFAUTI NA IDADI ILIYOTOLEWA AWALI NA UONGOZI WA MELI HIYO KUWA ILIKUWA NA ABIRIA 295 WAKIWEMO WAFANYAKAZI KUMI WA MELI HIYO.

AIDHA TUME HIYO PIA IMEBAINI KUWA MELI HIYO ILISAJILIWA KINYUME CHA SHERIA NA HIVYO KUPENDEKEZA MSAJILI WA MELI HIYO BW. SEIF JUMA,  KUCHUKULIWA HATUA KALI ZA KINIDHAMU.

HATA HIVYO TAARIFA YA TUME HIYO IMETOAUTIA NA TAARIFA ZILIZOKUWA ZIKITOLEWA NA JESHI LA POLISI KUHUSIANA NA IDADI YA MAITI ZILIZOKUWA ZIKIPATIKANA SIKU HADI SIKU.

KATIKA RIPOTI YA TUME HIYO, IMESEMA KUWA WATU 81 WALIPOTEZA MAISHA TOFAUTI NA TAARIFA ZILIZOKUWA ZIKITOLEWA NA JESHI LA POLISI KUWA HADI KUFIKIA TAREHE 11/8/2012, IDADI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA ILIKUWA NI 143.

MAITI ZA WATU 222 ZILIPATIKANA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MWAMBAO MWA BAHARI KWA UPANDE WA ZANZIBAR NA NYINGINE 21 ZIKAPATIKANA MKOANI TANGA.

TUME HIYO ILIYOKUWA IKIONGOZWA NA JAJI WA MAHAKAMA KUU MH. ABDRUHAKIM AMEIR ISSA, PIA IMETOA MAPENDEKEZO KUWA WATU WATANO AKIWEMO MMILIKI WA MELI HIYO BW.SAID ABDAHAMANI JUMA NA NAHODHA BW. MUSSA MAKAME MUSSA PAMOJA NA MENEJA MKUU WA KAMPUNI YA SEA GALL INAYOMILIKI MELI YA SKAGIT BW. OMARI MNKONJE WASHITAKIWE MAHAKAMANI.

WENGINE WANAOTAKIWA KUSHITAKIWA NI NAHODHA WA MELI HIYO BW. MAKAME MUSSA NA MHANDISI WA ZAMU WA MELI HIYO.  

MELI YA MV SKAGIT ILIZAMA TAREHE 17/7/2012 KATIKA BAHARINI KARIBU NA KISIWA KIDOGO CHA CHUMBE NA KUSABABISHA VIFO NA MANUSURA WA ABIRIA WALIOPANDA KATIKA MELI HIYO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...