Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro,Hajjat Mwatumu Malale (katikati) akiwa ameketi jukwaani na viongozi wengine wa Chuo Kikuu hicho,wakati wa sherehe ya mahafali ya tano ya Chuo hicho yaliyofanyika siku ya Novemba 17, mwaka huu.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro ( MUM) Hajjat Mwatumu Malale ( kushoto ) akimkabidhi mmoja wa mwanafunzi bora kimasomo wa Chuo hicho ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja wakati wa sherehe ya mahafali ya tano yaliyofanyika siku ya Novemba 17, mwaka huu kwenye viwanja vya Chuo Kikuu hicho.
Mwandishi wa Habari wa kituo cha Televisheni na Redio Abood, Abeid Dogoli ( wa kwanza kushoto) na wezake Mohamed Mohamed ,ambaye ni mfanyakazi wa Televisheni ya Zanzibar (ZBC) na Redio Zanzibar ,sambamba na Hamisi Mwesi , mfanyakazi wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ - Mazao) ( Mzinga) baada ya kutunukiwa Shahada ya kwanza ya Sanaa na Mawasiliano ya Umma kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro ( MUM) Hajjat Mwatumu Malale ( hayupo pichani) Novemba 17, mwaka huu katika viwanja vya Chuo Kikuu hicho.
Baadhi ya wahitimu wa shahada ya kwanza la ualimu.
Baadhi ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro wakifuatilia hotuba.Picha na John Nditi,Globu ya Jamii- Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Huyo mwanafunzi bora (mwanamke) aliyejifunika jumla huku akikabidhiwa zawadi, kulikuwa na haja gani ya kumpiga picha wakati na yeye hawezi kujitambua? Hakuna mtu anayeweza kumjua yeye ni nani kwa kuangalia PICHA.

    ReplyDelete
  2. ALHAMDULILLAAAH.
    MAFANIKIO HAYA YANATUTIA MOYO SANA WAFUASI WA UISLAMU. INSHAALLAH MATUNDA YA VYUO VIUKK VYA KIISLAMU YASAMBAE NA KULETA MANUFAA KWA JAMII YA WAISLAMU TANZANIA NA NCHI JIRANI. TUMESUBIRI SANA, LAKINI HATIMAYE HERI IMEVUTIKA.
    WAHITIMU, HASA WA SHAHADA YA UALIMU, ENDELEZENI KUSAMBAZA ATHARI ILI KUUSAMBAZA UISLAMU. TUENDELEZE JUHUDI ZA KUANZISHA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI NYINGI ZA KIISLAMU ILI KIKAZI CHETU NA TAIFA KWA JUMLA LINUFAIKE.
    TAKBEER...ALLAAHU AKBAR!

    ReplyDelete
  3. Michuzi unasema mhitimu ambaye jina lake halikuweza kupatikana? utapataje jina wakati huyo mwanamama kajifunika uso mzima kiasi kwamba siyo rahisi kumfahamu.

    ReplyDelete
  4. Nyinyi mnaotaka kumfahamu huyo mwanafunzi bora, mkashamfahamu ili iweje!!?

    ReplyDelete
  5. Watu wakware mwanawane utawaona.

    ...Ohhh kajufunika hatumwoni, tutajua yeye ni nani, ohhh , ohhh!.

    ...mumuzeoweya kuanikiwa migongo wazi, makwapa wazi, mapaja wazi, vifua wazi na vitovu wazi eee?

    Mmezoa timu za mauzo wanaoanika miili yao ili muweze kula kwa macho.

    Hapo kwa mwanamama dowezi wakubwa mmegonga mwamba.

    Anayeruhusiwa kumuona ni muweme tena wakiwa chumbani!!!

    ReplyDelete
  6. ehhhh weee vipi kwani umeambiwa hiyo fashion show. hapo umekosa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...