THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Hii vipi kwa timu yetu ya Taifa??

Mdau Alex Kajumulo ametuletea hii akitana wadau muipitie na kuona kama inafaa kuwa UZI wa  timu yetu ya Taifa (Taifa Stars).Wadau mnasemaje juu ya hili??


Kuna Maoni 31 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  SIO MBAYA Ila chata yake sio muhimu kwa kweli

 2. Anonymous Anasema:

  ina too much makorokocho!

 3. Anonymous Anasema:

  Inafaa 100%. Ni best kiliko zote nilizoona

 4. beny Anasema:

  ipo fresh sio mbaya akapewa dili la kutegeneza....tuache unafiki na majungu

 5. Anonymous Anasema:

  Mbaya mnoooooo!

  Hivi ni lazima kuweka rangi zote za bendera kwenye jezi zetu za timu ya Taifa??!!!

 6. Anonymous Anasema:

  mimi naona rangi nyeusisi aweke itapendeza.hiyo inaonekana kama imefanana na jezi ya zanzibar.mimi sijaipenda.

 7. Anonymous Anasema:

  Upangaji wa rangi bado ni tatizo sugu. Jezi zinawekwa rangi zoote mpaka inachukiza.Hata kama unataka kutumia rangi zote mpangilio uwe simple. kuweni wabunifu kidogo.
  Mzozaji.

 8. Anonymous Anasema:

  rangi nyeusi ambayo ni rangi muhimu haimo hivyo HAIFAI !

  asante !

 9. Anonymous Anasema:

  Hii haifai kuwa jezi ya Taifa kwa kuwa jezi haina rangi nyeusi ambayo iko kwenye bendera yetu

 10. Anonymous Anasema:

  Hiyo nembo yake(KAJUMULO)inatia shombo hapo vinginevyo poa tu!

 11. Anonymous Anasema:

  kajumulo ni mbuga gani ya wanyama TANZANIA? au unauza sura

 12. Anonymous Anasema:

  Tunaweza kutengeneza jezi ya taifa kwa kombinashen 24. Kumbuka hesabu za form four the combination and permutation. Bendera yetu ina rangi 4 kwa hiyo ni 4X3X2X1.

 13. Anonymous Anasema:

  vilaka vingi bana hiyo ssiyo afadhali hata zingine,kwani hiyo nayo kama zile zingine tu

 14. Anonymous Anasema:

  Lete, lete, lete, lete, lete!!!

  Alex Kajumulo bwana kaka,

  Fanya mambo uzi unafaa kabisa huo lete lete lete!

  Kama unavyoona brother Kajumulo Kikosi chetu cha Taifa kiko hoi bin taabani kwa upande wa nyuzi!!!

 15. Anonymous Anasema:

  BABU KAJU NAMKUBALI SANA SANA KTK VIFAA VYA MICHEZO.. HII SIO MBAYA LAKINI NAONA HIZO RANGI MBILI (NJANO) ZA KARIBIA NA SHINGONI UNGEZITOA..
  SHUKRAN

 16. Anonymous Anasema:

  Yaelekea alitaka kuinclude rangi za bendera ya taifa. Lakini nadhani amesahau rangi yetu ya asili, nyeusi.
  Hata hivyo nampa big up kwa kujaribu..

 17. Anonymous Anasema:

  Maoni yangu.Si mbaya lakini yafuatayo yangerekebishwa.
  1.Nembo zake(kajumulo) zimekuwa nyingi mno kama vile siyo ya taifa bali ni ya kajumulo stars.Apunguze hata kama ni mdau mkubwa.
  2.Rangi za bendera ya taifa hazijakamilika.Zingine hazipo.
  Ni hayo tu

 18. Anonymous Anasema:

  tunaomba kajumlo, angalie wapi pa kuweka rangi yetu nyeusi.

 19. Anonymous Anasema:

  nimeshasema mara kadhaa. Nembo ya TFF inabidi ipitiwe na wataalamu. Hii nembo haina hadhi kabisaa...imekaa kichovu sana. Kwana kuna ubaya gani ku-adopt nembo mpya? Wapeni vijana kazi wawaletee nembo nzuri ya TFF hii nembo ni vurugu tupu haina hadhi ya kitaifa. Kuna wadau wengi wanaweza kuanzia hapo. Kwa ujumla hii Jezz bado inatakiwa kazi kiasi...!!bado haijavutia sana....!!

 20. Anonymous Anasema:

  kwani uzi wa sasa una shida gani? MBONA uzi huu una nembo ya Kajumulo badala ta Taifa stars? Halafu mbona uzi huu hauna rangi nyeusi? Mi nilidhani Mr. Kajumulo si raia tena wa tz!

 21. Anonymous Anasema:

  Hapana,haifai.

  David V

 22. Anonymous Anasema:

  Ni Nzuri lakini naona rangi nyeusi inakosekana, kwa hiyo nadhani ingwekwa katikati ya rangi ya njano ya pembeni. Yaani punguza size ya strip ya njano ili ziwe mbili halafu katikati ndio hiyo nyeusi

 23. mlay Anasema:


  infaa sana ila tungeomba tuonee na huko mgongoni kuna rangi na alama gani?? je mtu binafsi ukitaka kupata nakala yako utapataje?? thanks babu kajo for your contribution to our country.

 24. Anonymous Anasema:

  Its a good thing to see a Tanzanian doing great thing.Keep it up bro!uzi uko poa sana na ninaunga mkono hoja.Mungu ibariki nchi yetu

 25. Anonymous Anasema:

  Hiyo KAJUMULO ndio imechukua nafasi ya Nike, Adidas, Puma...siyo?

  Mimi naona siyo sawa, iwekwe TANZANIA, maana kutokana na uwezo wetu waTZ, kesho atatokea MURJI, CHUDASAMA, MUSHI, MWASAKAFYUSI, RAMIA, CHOLO...

  JE, SI ITAKUWA VURUGU MECHI?

 26. Anonymous Anasema:

  Wabongo 2napenda Kukosoana Saana ...Majungu Meengi..Uzi Uko Poa..Bob Kaju Mwaga Nyuki...

 27. Anonymous Anasema:

  Mpangilio wa rangi mbovu.!!!...sio lazima kuwa na rangi zote za bendera ya Tanzania kwenye jezi. Uzi huo haufai..!!

 28. Anonymous Anasema:

  Si lazima kila rangi iliyopo kwenye bendera iwepo kwenye jezi thts y inaonekana too complicated!

 29. Anonymous Anasema:

  Mimi niulize timi ya taifa jee taifa gani ninavyofahamu mimi TANZANIA ni muungano wa nchi mbili yaani ZANZIBAR na TANGANYIKA na ZANZIBAR tuna timu yetu bendera yetu na wimbo wetu wa Taifa sasa hili laplap la hapo juu sielewi la taifa gani au ndio Tanganyika any way ikiwa ni hivyo why dont you made it clear and call it Tanganyika star. Acheni ujinga huo mtu hakatai asili yake.

 30. Anonymous Anasema:

  Pengine mimi macho yangu hayaoni rangi vizuri lakini ninaiona rangi nyeusi chini ya rangi ya manjano au macho yangu? S.C. Toronto, Canada

 31. Anonymous Anasema:

  Siyo kwamba wabogo wanapenda kukosoa na majungu mengi kama mchangiaji mmoja alivyosema, aliyeiweka jezi hiyo kwenye mtandao alihitaji watu watoe maoni yao ili kama kuna marekebisho yafanyike. Tafadhari heshimu mawazo ya wengine hata kama yanapingana na yako. Ndg Kajumulo, nembo yako haihitajiki kwenye jezi ya timu ya taifa iondoe