KLABU ya Yanga imeingia mkataba na kampuni ya Pecha Media Health Promotion kwa ajili ya kutengeneza kalenda za klabu hiyo za mwaka ujao 2013 na inategemea kuvuna shilingi milioni 150,000,000 kupitia kalenda hizo.
Katibu mkuu wa Yanga Laurance Mwalusako alisema kuwa  kampuni hiyo tayari imeshatengeneza kalenda 100,000 kwa kuanzia ambapo zitauzwa siku ya mkutano mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika kwenye ukumbi wa PTA uliopo Sabasaba jijini Dar es Salaam.
"Tuna bidhaa nyingi ambazo watu wanauza kiujanja ujanja bila ya kuingia mkataba na sisi sasa tumeamua rasmi kuwavalia njuga watu hao na yeyote atakayepatika anauza bidhaa zetu visivyo halali tufamfikisha kwenye jeshi la polisi.
Alisema kalenda hizo zitauzwa kwa shilingi 5,000 kila moja na hiyo itasaidia kuinua kiuchumi klabu hiyo ambayo alidai kuwa imedhamiria kufika mbali kimaendeleo.
Naye mkurugenzi wa Pecha Media Nassib Limira alisema wameamua kuingia mkataba na Yanga akiamini kuwa wanachama na mashabiki wa klabu hiyo watawaunga mkono kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameisapoti klabu hiyo ambayo itanufaika na shilinig 1500 kwa kila kalenda na iwapo zitauzwa kalenda zote 100,000 basi Yanga itavuna shilingi milioni 150,000,000.
Alisema kampuni yake itavuna shilingi 400 kwa kila kalenda wakati wauzaji watapa shilingi 300 kwa kila kalenda na gharama nyingine zitabaki kuwa za uzalishaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kalenda ya Yanga,

    Iwe na kumbukumbu ktk tarehe zake kwa miaka balimbali iliyopita ambayo Mabao ya Yanga yalielekezwa Simba SC.

    Katika terehe hizo za kumbukumbu na miaka yake ni muhimu idadi ya mabao yawekwe na wafungaji wake!

    ReplyDelete
  2. Ukurasa mmoja uoneshe twite akipokea hela za simba

    ReplyDelete
  3. Katika kalenda msisahau kuweka mabao 6 - 0 ya zamani na 5 - 0 ya hivi karibuni, angalau tukumbuke nani walihusika kuleta dhahama hiyo jangwani!!!

    ReplyDelete
  4. Mwana Msimbazi Mtani wangu anony Wed Dec 05, 02:39:00 PM 2012 hayo mabao 6-0 na hayo mengine 5-0 tuliyachomoa kwa ile gharama mliyotoa (35 Milioni) kwa Manunuzi ya Twite kama Mdau wa pili (2) anavyosema akipokea hela zenu matokeo yake sasa yupo anachezea YANGA S.C,,,

    Je nani ni zaidi?

    ReplyDelete
  5. Mdau wa tatu wa Simba S.C anonymous wa Wed Dec 05, 02:39:00 PM 2012

    ...Ni muhimu kalenda ionyeshe ile Jezi ya Twite No.4 iliyoandikwa (R,,,GE)!

    Hapo ndio kuonyesha kuwa mimi Yanga S.C nimezaliwa ,mwaka 1936 na wewe Simba S.C umezaliwa mwaka 1938 hivyo nimekupita miaka miwili kiumri!

    Hivi jamani Kulwa na Doto wanazaliwa siku moja lakini anayetangulia kuzaliwa ni Kulwa na ndio anatambulika ndiye mkubwa sembuse KWA NINI MIMI YANGA S.C NISIITWE MKUBWA KWAKO WEWE SIMBA S.C?, ni kuwa Kulwa kumzidi Doto kwa Dakika anapewa haki ya kuwa mkubwa , kwa nini na mimi nisipewe heshima yangu kwa kukuzidi wewe miaka miwili?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...