Mbunge wa Wawi Mhe. Hamad Rashid Mohamed akifurahia jambo na baadhi ya wabunge wa kamati ndogo ya wabunge kutoka Tanzania, Uingereza na Pakistani iliyoundwa wakati wa Mkutano masikilizano baina ya Mabunge duniani (IPU) na Umoja wa Mataifa kuangalia namna bora ya Mabunge kuyawajibisha Mashirika ya Kimatifa kutokana na kuingilia migogoro yenye uvunjifu wa Amani Duniani katika mkutano wa ushirikishwaji wa Mabunge katika njia za kuzuia migogoro, usuluhishi pamoja na namna bora ya kujenga amani duniani uliofanyika Mjini New York Marekani na kumalizika leo. 
 Senator wa Bunge la Pakistani Mhe. Mohammad Mohsin Khan Leghari akitoa mapendekezo ya kamati ndogo ya wabunge kutoka Tanzania, Uingereza na Pakistani iliyoundwa wakati wa Mkutano masikilizano baina ya Mabunge duniani (IPU) na Umoja wa Mataifa kuangalia namna bora ya Mabunge kuyawajibisha Mashirika ya Kimatifa kutokana na kuingilia migogoro yenye uvunjifu wa Amani Duniani katika mkutano wa ushirikishwaji wa Mabunge katika njia za kuzuia migogoro, usuluhishi pamoja na namna bora ya kujenga amani duniani uliofanyika Mjini New York Marekani na kumalizika leo. Kulia kwake ni Mhe. Hamad Rashid Mohamed na Mhe. Craig Whittaker kutoka Bunge la Uingereza
 
Katibu Mkuu wa IPU Anders Johnson akimpongeza Mhe. Hamad Rashi Mohamed kwa mchango wake uliosisimua mkutono huo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wanamna bora ya kushirikisha Mabunge yote duniani kushiriki katika njia za kuzuia migogoro, usuluhishi wake pamoja na namna bora ya kujenga amani duniani uliofanyika Mjini New York Marekani kwa siku mbili na kumalizika leo
Mhe. Hamad Rashid Mohamed akitoa mchango wake katika Mkutano wa wa siku mbili wa masikilizano baina ya Mabunge duniani (IPU) na Umoja wa Mataifa kujadili namna bora ya Mabunge yote duniani kushirikishwa katika njia za kuzuia migogoro, usuluhishi pamoja na namna bora ya kujenga amani duniani uliofanyika Mjini New York Marekani na kumalizika leo. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mh. Hamad Rashid Moh'd nimependa jinsi ulivyowakilisha Bunge la Tanzania kwa kutumia hoja iliyojaa uelewa wa msuala haya ya amani barani Afrika.

    Pia Ankal utubandikie pia jinsi wabunge wetu ktk Bunge la afrka mashariki tuone hoja zao juu ya masuala mbalimbali Afrika mashariki na hususan kwa mtazamo wa Tanzania kwani shughuli za EALA (Bunge la Afrika Mashariki) ni kiduchu sana.
    Mwananchi
    Namanga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...