Wananchi wa Mwanza wakiipokea treni ya Shirika la Reli Tanzania(TRL), kwa ujumbe wa Mabango wakatii treni hiyo ilipowasili Mkoani Hap oleo mchana. Treni hiyo ilisitisha huduma zake tangu Mwaka 2009, Imeanza safari zake rasmi kwa mabehewa Sita, likiwemo moja la daraja la Kwanza. Treni hiyo itakuwa ikifanya safari zake Mara mbili kwa Wiki.
Baadhi ya Abiria wa wanaotumia usafiri wa Treni ya Shirika la reli Tanzania (TRL), waliotokea jijini Dar es Salaam ijumaa kuelekea Mkoani Mwanza wakiwa ndani ya behewa la Daraja la Tatu kama walivyokutwa leo asubuhi .Treni hiyo imeanza safari zake kutokea Dar kwenda Mwanza.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba(mwenye suti Nyeusi),akiwa ndani ya Mabehewa ya Treni ya Shirika la Reli Tanzania(TRL)leo Asubuhi wakati alipoipokea treni hiyo iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Slaam.Treni hiyo ya kwenda Mwanza imeanza rasmi Ijumaa kutokea Dar kwenda Mwanza baada ya kusitisha huduma zake tangu mwaka 2009.
Wananchi wa Mkoani Mwanza wakipunga mkono kuashiria furaha yao kwa kuanza kwa Safari za Treni ya Shirika la Reli Tanzania (TRL).Treni hiyo imeanza safari zake ijumaa kwa kutokea Dar es Salaam kuja Mwanza.
Baadhi ya Abiria wanaotumia usafiri wa Treni ya Shirika La Reli Tanzania(TRL),wakishuka katika Stesheni ya Mwanza Leo Mchana kutokea dare s Salaam.treni ilisitisha safari zake kwenda Mwanza mwaka 2009 na Ijumaa ilianza safari kutokea Dar kwenda Mwanza.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba, akisisitiza wafanya biashara waliojenga vibanda na kufanyia biashara karibu na Miundombinu ya Reli katika eneo la stesheni ya Reli Mwanza mpaka Maeneo ya Mamlaka ya Bandari(TPA),kuhama katika maeneo hayo kama Sheria ya Reli inavyoelekeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

 1. nchi yangu kweli bado ni maskini sana...dah nikiona hizi picha machozi yananilengalenga...kweli kwa karne ya 21 tunatumia usafiri ulichoka hivi!!.na watu wanafurahi maana hawajawahi kuona upande mwingine wa dunia wanavyoishi..!.sijui mafisadi wakiona hivi wanajisikiaje kuona ndugu zao wa damu wakiteseka namna hii ilihali wao wameficha hela ughaibuni?

  Nimeumia sana kwa kweli.

  mdau - canada

  ReplyDelete
 2. Vipi kuhusu 'treni ya mwakyembe TAZARA'maana nayo inahitaji kufuatiliwa ili usafiri wa TAZARA uwe mfano wa treni ya uhakika wa usafiri Tanzania na Zambia.
  Mdau
  Tunduma

  ReplyDelete
 3. He! kumbe safari zilikuwa zimesimama, tangu lini. Nani alihujumu. sasa tumejipangaje kuzidumisha. Mizigo yote mizito isafirishwe kwa guds treni chini ya ulinzi. Nilikuwa sikumuelewa nyerer aliposema kuwa ubepari ni unyama.

  ReplyDelete
 4. Hongera Mhe. Dr.Mwakyembe na Serikali kwa huduma hii muhimu sana kwa watu wa kawaida.

  Mara nyingi inakuwa vigumu kuwapata watu mahiri kutokana na wengi wasiostahili kujipenyeza penyeza.

  Hatukujua kama tuna watu wanaofaa kama safu iliyopatikana ya Mawaziri kama akina Mhe.Mwakyembe, Mhe.Magufuli ,Mhe.Kagasheki na wengineo ktk Mawaziri!

  ReplyDelete
 5. Mdau wa tatu hapo juu Dec.10 10:AM naungana nawe kabisa kwa msemo wa mwalimu kuwa ubepari ni unyama,mabepari hawajali kuwepo kwa wanyonge.Sasa tunaweza kuona jinsi waziri alivyopigana kurudisha treni kazini,lakini hebu angalia hizo hali za viti vya abiria wa daraja la 3,inasikitisha jinsi viti vilivyochoka bado hatujaona sehemu nyingine nyeti.Hivi jamani hata matengenezo madogo au marekebisho yanahitaji wizara kufanya?hapo ndiyo unaona jinsi ubeperi ulivyo unyama,wao kwao abiria wa 3rd class hawana maana sifikiri kama huko 1st class kuna hali kama tunayoiona hapo.Ilipasa matengenezo hayo madogomadogo yafanyike kabla ya huduma kuanza kwani uharibifu utakaoendelea utakuwa ni mkubwa na gharama zake kuwa maradufu ya ambavyo matengenezo hayo yangefanyika kabla.Lakini kwa kampuni ya kibepari hilo hawalipi umuhimu wowote kwani walala hoi ni binadamu wa class ya chini kwao.
  Kweli ubepari ni unyama,maslahi mbele human values hakuna.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...