Mkurugenzi wa Kampuni inayojenga gati ya Kipili, mkoani Mpanda, Bw. Emmanuel Mashanche akimuonyesha Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Charles Tizeba eneo la mradi wa Ujenzi wa Gati hiyo kulingana na Mkataba aliongia na Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA). Naibu Waziri alitembelea mradi huo Mwishoni mwa wiki hii kuangalia maendeleo yake.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo kwa mkandarasi aliyepewa kazi ya kujenga Gati ya Kipili, Wilaya ya Mpanda, Bw. Emmanuel Mashanche(kushoto kwa Waziri)na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Mhandisi Senzige (mwenye flana nyekundu). Naibu Waziri alitembelea Mradi huo mwishoni mwa wiki hii na kuwaagiza Mamlaka ya Bandari kuhakikisha Ujenzi huo unaisha kwa Wakati.
Mafundi waliopata zabuni ya kujenga Gati ya Kipili, mkoani Mpanda, wakiendelea na ujenzi wa Gati hiyo kama walivyokutwa Mwishoni mwa wiki.
Muonekano wa Hatua aliyofikia na Mkadarasi aliyepewa Mradi wa Kujenga gati ya Kipili, Wilayani Mpanda, kama ulivyokutwa mwishoni mwa wiki hiii.
Naibu waziri wa Uhcukuzi,Dkt Charles Tizeba(mwenye koti la kaki),akiongea na wanakijiji cha Karema, Wilaya ya Mpanda, alipotembelea Bandari ya Karema mwishoni Mwa Wiki hii.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt Charles Tizeba, akijaribu ubora wa Kyson ambalo linatumika kujengea gati ya Karema, Wilaya ya Mpanda, mwishoni Mwa Wiki. Naibu Waziri alitembelea mradi wa Gati ya Karema kuangalia maendeleo ya Mradi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...