THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KIJIWE CHA UGHAIBUNIKuna Maoni 16 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Nilipokuwa nikiwa shule secondary miaka ya 80 au enzi za Mwalim, kwenda ughaibuni ilikuwa ni kwa kusoma, kiserikali au kuzamia meli. Ubaharia ulikuwa deal kubwa enzi hizo. Kila mtu alipewa aka ya baharia katika vijana. Habari nyeti zilizokuwa zililetwa kuhusu hawa mabaharia hazikuwa nzuri, wengi wao wakirudi Bongo huwa na afya nzuri na pesa lakini baada ya muda hufilisika na wengi huwa wapiga virungu wazuri. Baadae miaka ya 80 mwisho ikaingia biashara ya unga. Mpaka miaka ya 90 katika ikawa wauza unga ndio ndio deal. Wauza unga wakawa na pesa sana mwisho wakaishia kuwa mateja. Miaka ya 90 kati mkapa 2005 ikawa zamu ya wakimbizi. Ukimbizi ukawa ndio deal kila kijana anatafuta nauli angie UK kujiripua. Tangu ilikuwa unaingia UK bila ya viza mpaka ikawa kwa viza. Watu wameuza majumba kusafiri, hata watoto wa wabunge na mawaziri na vigogo wakajumuika katika kuwa wakimbizi. Hata wasomi nao pia wakajiunga na wimbi la kujiripua. Kuna watu wengi wamepata uraia wa ughaibuni wanakuja Bongo na singilendi vacation. Lakini watu hawa wote hakuna aliyetajirika akawa kama Bill Gate. Zaidi sasa Bongo kumeingia roho mbaya na kutokuaminiana baina ya watu hata wa familia moja. Nilichojifunza mimi ni kuwa maisha ni popote mtu alipo afanye bidii ili afanikiwe. Kama upo Bongo basi fanyakazi au soma kwa bidii ili utajirike. Maisha ya ujanja ujanja hayana mwisho mzuri. Nilipokuwa naomba viza ya UK niliwakuta Wazungu watatu wanaomba nao viza. Mmoja alikuwa ni mzee sana mgonjwa na walikuwa na passport za Bongo. Jamaa mmoja aliwauliza sasa nyinyi vipi wakasema sisi Wabongo bwana tupo hapa kabla ya uhuru tumezaliwa hapa na huyu baba yetu tunampeleka matibabuni tu UK.

 2. Anonymous Anasema:

  maneno ya wabeba box ya kujipa matumaini,nyi kalagabaho na maisha ya kujidanganya, eti hapa 'mtoni'.mnachoogopa kurudi bongo ni shule,utaanzia wapi?mnachofaidi huku ni umeme wa uhakika na barabara nzuri lakini bongo ni tamu asikwambie mtu lakini ukiwa umejipanga.kila la heri la box zenu hahahahahha

 3. Anonymous Anasema:

  The first one was on point! This one came out a bit more Ignoramos, as if ya'll tried a bit too hard!

 4. Anonymous Anasema:

  Jamani wenzenu hilo chicha huwa wanazuga tu wakiwa kwenye issues kama hizo mazozijaribu nyinyi. Nyie mnapiga chicha la kweli matokeo yake mna sound nonsensical! Lose the damn boose, mueleweke jamani! Ya mwanzo mlijitahidi, ilikuwa inaelimisha na ku entartain at the same time. Hii naona mnatukana tukana tu na kuongea vitu visivyo na kichwa wala miguu. Wise up fellas!!

 5. Anonymous Anasema:

  kwa uzoefu wangu, afadhali wenzetu hawa wa visiwani wanapokutana ughaibuni, mtu unaingia leo wenzako wanakuweka chini na kukupa michongo, au wanapokuona hueleweki huwa wanakuuliza ili nawe uwe ktk mstari. sisi wabara tuna tabia ya kukwepanakwepana huku mtoni pale unapomuona humjui au unamuhisi mwenzako anaishi vp. chuki tulizonazo inafika hata wakati mtu anamchomea mwenzie mpaka anapigwa bomba. na imefika wakati hapa kwa bibi wabongo huwa wanawachomea wenzao kwa wazee ili waharibikiwe na mambo yao. Tunawachukia bure wapopo, wadosi lakini in real term huwa wanasaidiana sana na hawana tabia ya kuwakatisha tamaa jamaa zao pale wanapokuwa wanajaribu maisha. hebu tujiulize imekaaje hii? na au kuna laana gani? wengina wanafikia hata hatua ya kuzikana pesa, ugomvi katika sherehe zetu hasa pale wanapokuja wasanii kutoka nyumbani.

 6. Anonymous Anasema:

  Nadhani mnaleta mzaha usio na maana, mnaonekana watu wazima lakini ni uzima wa ukomavu wa sura na wala siyo fikra. Popote mtu anaweza kufanikiwa ilimradi awe na malengo na atie bidii katika malengo yake. Watu mmekaa na vijichupa vya pombe ya $ kidogo, maongezi na misemo ya kihuni kwa hakika mko kijiweni na daima watu wa kijiweni mwisho wao kijiweni. Wenzenu mbona wapo huko huko na wengine uk wanafanya mambo ya maana ninyi vipi? Mnaendekeza starehe zisizo na mpangilio halafu mnalalamika. Achaneni na hii habari fanyeni kitu cha maana

 7. Anonymous Anasema:

  Hawa jamaa inaonekana hawana elimu kabisa hata mazungumzo yao hayana hata maana.Mbona kuna watanzania wengi tuu wenye maendeleo??na mbona kuna watanzania wengi wengi wanapendana kama ndugu...mie hawa jamaa siwaamini kabisa...

 8. Anonymous Anasema:

  Du am speechless.Hawa jamaa IQ yao is about 30 or 40.But i believe these guys are better off here in US than Tanzania.Tanzania with this level of ignorance wangekuwa either wapiga debe, au ndio watu wa kubeba mizigo kariakoo.
  Watu kama hawa hata ukimpa 1 Million $ today , atakufa maskini.

  Kuna ule usemi watu wanasema kuna watu kufika Marekani tu kwao they have made it.Sasa ule usemi ndio exactly una reflect hawa jamaa.
  Mungu wabariki..ila msithubuthu kurudi bongo..bongo land will eat you guys alive.

  Mdau DC

 9. Anonymous Anasema:

  Sio watu wanaogopa unapokuwa nchi zenye demokrasia hata nafsi yako inabadiriki matumaini, na taratibu zako za kimaisha ubadirika kama unavyojua binaadamu ameumbwa na kusahau na haya ndio mabadiriko hivyo unapokuwa bongo unajikuta unapwaya na taratibu zima ya maisha

 10. Anonymous Anasema:

  msiwatetee wabongo kabisa waliopo USA, wengi waliokuja zaidi ya miaka 10 iliyopita ndio tatizo kuu la chuki na kutopenda maendeleo ya wenzao hasa wenye mda mfupi na wanaoonyesha kufanikiwa. Mimi mwanafunzi na nimefika hapa miaka michache sana iliyopita hata US sijaitambua vizuri japokuwa nimefanikiwa kuishi majimbo matatu kwa nyakati tofauti. Nimeshuhudia mengi sana ya ukarimu na ubedhuli wa watanzania wenzangu, nimeishi na watanzania ambao wanaumoja na kuishi kama ndugu katika majimbo mawili yenye idadi ndogo ya watanzania. Miezi kadhaa nikabahatika kufika katika jimbo lingine lakini nilishindwa kuamini mtu anapokwambia hamfahamu Mtanzania mwenzake kisa kamzidi kimafanikio. Matatizo haya yapo hasa katika majimbo yanayosifika kuwa na watanzania wengi pamoja na kuendeleza starehe.

 11. MATANGALU Anasema:

  Hawa jamaa siyo kiwakilishi cha watanzania waliopo ughaibuni. Ukisikiliza maongezi yao wanalaumu watanzania wenzao kwamba wana roho mbaya wakati wao wenyewe wanatumia nguvu zao zote kukatisha tamaa wenzao. Hiyo ndiyo roho nzuri kwa mujibu wa watu hawa wawili.

  Na huyu mwingine anayesema kwamba wabongo wengi waliopo marekani Bongo walikuwa dereva wa sinia, sijui huyu naye anatoka katika familia ya aina gani. Mtu yoyote anayetoka katika familia yenye nidhamu na yenye kulea watoto wao, basi lazima kila mtoto apitie hatua hiyo ya "udereva wa sinia". Huyu jamaa inaoneka anatoka katika familia ambayo ukishafika miaka tisa unatakiwa utoe mchango wa hela ya kula nyumbani. Sidhani kama hicho ni kitu cha kujivunia.

  Kuhusu vijana wadogo mliopo bongo, kama ukiona milango yako bongo imefungwa basi jaribu ughaibuni kama unaweza, na usiwasikilize hawa jamaa ambao wameshashindwa sasa wanataka kuwakatisha tamaa wenzao ili nao washindwe kama wao. Na hiyo ndiyo roho mbaya ya wabongo.

 12. Anonymous Anasema:

  ushamba unawasumbua, kutokujua mambo mengi na kutokuzoea mazingira, fikra za kimaskin. Reality hata bongo kama unajipanga vema life its there for real!.
  Wa kwanza kuongea kidogo he was about to hit the point lakin kazi kwa bidii ndio msingi wa maisha na kupendana....mungu awasaidie kuwaamsha.,
  mdau japan.

 13. Anonymous Anasema:

  Maisha popote pale muhimu ni subira kwa tulioko huku uk mimi naona tupo fresh tu!! hiyo hiyo pesa ya kubeba box ndio tuliojengea huko nyumba na mambo mengine!! na jambo jengine la msingi ni kuweka msingi mzuri kwa watoto kwani wanapata masomo mazuri huku ambayo yatawasaidia popote watakapo kwenda kuishi kwani huwezi kulinganisha vyeti vya uk na vya bongo!! huu ndio ukweli kataa au kubali!! ukitaka kulijuwa hili angalia watoto wa viongozi kote Duniani watoto wao wanasoma wapi???? Nafikiri jibu unalo!!

 14. Anonymous Anasema:


  Sasa basi Obama katangaza strict immigration policies hakuna kazi tuone watafanyaje huko

  Ila wanaongea ukweli kabisaa sema watu kinao wagusa ndo mnajifanya kuponda hapo ni 100% true wabongo tumezidi kua wachoyo na tamaa ndo maana sio U.S peke yake hata china the same case

 15. Anonymous Anasema:

  watu tupo wa aina nyingi na malengo tofauti elimu pia tunatofautiana sasa tunapofika na kutafuta maisha ugenini kwa ninituwe na lengo moja au tuwe kama tumetumwa na baba ua mama wa taifa tunalotoka kuwa wanangu mkifika huko mfanye abcd
  mimi naona tusiwahukumu hawa wenzetu nimeona chupa za kijani sio mali ya ccm ni mali ya mholandi 'heineken'
  sasa tunategemea maoni gani baada ya kunywa hili togwa.
  tufurahi tu jamani.
  mdau, mid- west usa.

 16. Anonymous Anasema:

  LOOOOH MWENYEZI MUNGU NAOMBA UWA HURUMIE RAFIKI ZANGU HAO KAMA ULINYO NIHURUMIA KINITOA PUMBA