TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha
5(51) cha Sheria ya Majukumu ya Mawaziri The Ministers (Discharge of Ministerial
Functions)Act, sura ya 299 ameanzisha Chombo cha Kusimamia Ufuatiliaji
wa utekelezaji wa program na Miradi ya Maendeleo kwenye Maendeo ya Kimkakati ya
Kitaifa (National Key Result Areas) kinachojulikana kama “President’s
Delivery Bureau (PDB)”.
PDB itakuwa chini ya
Ofisi ya Rais, Ikulu na itakuwa na majukumu yafuatayo:-
·
Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa
Programu na miradi kwenye Maeneo ya kimkakati ya Kitaifa yanayohitaji matokeo
ya haraka.
·
Kuwezesha ufafanuzi wa kina na program
kwenye maeneo ya Kimkakati ya Kitaifa yanayohitaji matokeo ya haraka.
·
Kuwezesha na kufanikisha kuanzisha program
na miradi kwenye Maeneo ya Kimkakati ya Kitaifa yanayohitaji matokeo ya haraka.
·
Kuwezesha kutambua na kuainisha Maeneo ya
Kimkakati ya Kitaifa yanayohitaji matokeo ya haraka.
·
Kusaidia kutoa uchambuzi na mapendekezo ya
namna ya kukabiliana na changamoto maalum za utekelezaji.
·
Kushirikisha umma kwenye Program na miradi
iliyoainishwa kwenye maeneo ya kipaumbele.
·
Kuandaa taarifa za utendaji kwa kipindi
maalum kwenye Maeneo ya Kimkakati ya Kitaifa na kuziwasilisha kwenye mamlaka
husika.
·
Kutoa ushauri wa kitaalam wa ndani na
kuishauri Serikali kwenye maeneo ya Kimkakati ya Kitaifa.
·
Kupanga na kusimamia uendeshaji wa shughuli
za ‘Labs’.
·
Kuwezesha usimamizi wa mikataba ya utendaji
kwa Mawaziri wanaouhusika na program na miradi ya kipaumbele iliyo chini ya
Wizara zao.
·
Kuwezesha na kusimamia uandaaji wa
viashiria vikuu vya utendaji (Key Performance Indicators) vya
kitaifa na kiwizara kwenye program na miradi ya kipaumbele.
·
Kufanya uhakiki wa utendaji wa Mawaziri
kwenye Maeneo ya Kimkakati ya kitaifa yanayohitaji matokeo ya haraka.
·
Kuwezesha uhakiki wa utendaji wa PDB.

Ndugu Omari Issa ni Mtanzania mwenye
uzoefu mkubwa ndani na nje ya nchi, barani Afrika na duniani, kwenye sekta ya
umma na sekta binafsi, na kwenye ulimwengu wa biashahra na utendaji wa
makampuni makubwa ya kimataifa.
Mheshimiwa Rais anaamini kuwa uzoefu huo na utamaduni huo wa utendaji
katika sekta binafsi katika ngazi hiyo utakuwa mchango mkubwa na muhimu katika
siku za mwanzo za President’s Delivery Bureau na ubadilishaji wa utamaduni wa
utendaji Serikalini kwenye maeneo ya kipaumbele. Ndugu OMARI
ISSA alikuwa Mtendaji Mkuu wa kwanza wa “Investment Climate Facility for
Africa”.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
31 Mei, 2013
Omari Issa is a good choice to lead this new body, wish you all the best in this new challenge Omari.
ReplyDeleteHongera sana,kwa uteuzi,tunaomba mpatie ushirikiano ili tuone matunda yake.viongozi wengi wamekuwa mzigo kwa taifa kwa uawajibika ni mdogo sana.
ReplyDeleteGreat selection indeed . All the best PDB.
ReplyDelete