Bwana na Bibi Kanza.

Wapendwa wetu, ilikuwa siku, wiki, mwezi na hatimaye tarehe 01/05/2013 mmetimiza miaka minne (4) toka mtutoke kwa ajali ya gari katika hii dunia. Tunafarijika kwa sababu tuna Imani mpo pamoja nasi Kiroho siku zote.

Hakuna siku ipitayo kwetu bila kuwakumbuka kwa UPENDO, UKARIMU, USHAURI MWEMA, MSIMAMO BORA NA BUSARA ZENU. Hakika BUSARA ZENU zimekuwa dira na nuru katika maisha yetu. Tunaendelea kuwaombea na tutaendeleza yale yote mema mliyotuachia.

Daima mnakumbukwa na watoto wenu, Bright Kanza na Alvin Kanza, Mr & Mrs T. Kweka, Mr & Mrs G. Kanza, wadogo zenu wote, wajomba, shangazi, ndugu, jamaa na marafiki. Daima tutawakumbuka Milele.

Sisi tuliwapenda sana, lakini Mungu Baba wa Mbinguni aliwapenda nyinyi zaidi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe. Amen!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...