Mkurugenzi Mkuu wa Helvetic Solar
Contractors Eng. Patrick Ngowi akiwa na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhavile alipofika katika ofisi hizo mapema leo kwa ajili ya
mazungumzo na kuhojiwa katika kipindi cha Business Edition, kitakachorushwa
Ijumaa hii saa 2 na dakika 15 usiku, Capital TV.
Dar es
Salaam. 21 Mei, 2013.
Mkurugenzi Mkuu wa Helvetic Solar Contractors Eng. Patrick Ngowi ameendelea
kutoa rai kwa vijana nchini Tanzania kuwa na moyo na bidii ili kuweza kutimiza
ndoto zao za maendeleo na kujikwamua kiuchumi.
Eng. Ngowi ambaye pia ni mshindi
wa ‘Forbes 2013: 30 under 30: Africa’s Best Young Entrepreneurs’ alisema maneno
hayo mapema leo katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce
Mhavile alipofika kufanya ziara na mahojiano maalum katika kituo hicho.
“Vijana wa kitanzania wanafursa
nyingi sana katika nchi yetu, imefika wakati sasa vijana wajitambue kwamba
wanaweza kutimiza ndoto zao kadiri bidii zao zitakavyowatuma. Kwa mfano, mi
nilianza na mtaji wa shilingi milioni mbili, lakini hivi sasa nilipofikia
biashara yangu imekua na nimeweza kufanya maajabu makubwa katika soko ukizungumzia
swala ya nishati ya jua,” alisema Eng. Ngowi.
Aliongeza, “Kinachotakiwa ni kuwa
mbunifu katika biashara unayofanya, kuwa na ujasiri pamoja na umakini wa kile
unachokipenda na pale unapotaka kufika. Yote yanawezekana na kijana yeyote
anaweza fanikiwa.”
Pamoja na hayo Eng. Ngowi
aliwapongeza sana IPP media kwa mafanikio yao waliyopata katika kipindi chote
tangu kianzishwe, ikiwemo tuzo ya ‘Number 1 Super Brand’ katika Afrika
Mashariki hivi karibuni.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhavile alimpongeza kwa mafanikio yake na kumshukuru sana Eng.
Ngowi kwa ugeni wake.
Kampuni
ya Helvetic Solar Contractors ambayo Eng. Ngowi ni muasisi wake, mwaka jana
iliweza kushinda nafasi ya kwanza katika mashindano ya ‘100 Top Mid-Sized
Company in Tanzania.’ Mwezi Machi mwaka huu Eng. Ngowi aliweza kuorodheshwa
katika kundi la wajasiriamali bora 30 vijana barani Afrika wenye umri chini ya
miaka 30 ijulikanayo kama ‘Forbes 30 under 30:
Africa’s Best Young Entrepreneurs’.
Picha
na habari na Amani Nkurlu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...