Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali akiwa na ujumbe wa Wabunge toka Oman yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku sita ambapo pamoja na mambo mengine amesaini mkataba wa uanzishwaji wa ushirikiano wa Bunge la Tanzania na Bunge la Oman katika Maswala mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma jana.
Kaminisha wa Tume ya Utumishi ya Bunge Mhe. Abdulkarim Shah akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma jana.
Naibu Spika Mhe. Job Ndugai akimtambulisha Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah kwa Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali alipowasili Dodoma jana.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge Dodoma ambapo anafanya ziara ya kibunge ikiwa ni pamoja na kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya mabunge haya mawili.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda pamoja na Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali wakisaini mikataba ya makubaliano ya ushirikiano baina ya mabunge haya mawili.
Wakibadilishana mikataba ya Makubaliano.
Picha ya Pamoja Ujumbe wa Spika wa Bunge la Oman na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2013

    Waheshimiwa Masheikh wa Oman wanakubaliana na BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA!

    Mmeona wenyewe mnaodai ''ohhh Oman wanatuunga mkono kuhusu suala la kuuvunja Muungano'',,,KAMA MANENO HAYO NI YA KWELI MASHEIKH HAWA WA KISERIKALI WA HUKO OMAN WANGEKUJA HADI 'MJENGONI' DODOMA?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2013

    Waheshimiwa Masheikh wa Oman wanakubaliana na BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA!

    Mmeona wenyewe mnaodai ''ohhh Oman wanatuunga mkono kuhusu suala la kuuvunja Muungano'',,,Haya yatakuwa ni Madai ya kwenye Vijiwe vya Kahawa na Urojo),,,KAMA MANENO HAYO NI YA KWELI MASHEIKH HAWA WA KISERIKALI WA HUKO OMAN WANGEKUJA HADI 'MJENGONI' DODOMA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...