Kama umefikia Mkoani Ruvuma hususani wilaya ya Songea Vijijini,basi ni lazima utakuwa umepita katika Kijiji cha Peramiho ambapo kuna Kanisa hili kubwa la lenye historia ya kipekee.Hili ni Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Benedict Abbey lililopo ndani ya Kijiji cha Peramiho mkoani Ruvuma. Lilijengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita lakini ukiliangalia leo ni kama vile limejengwa jana.
Sehemu ya Kumbukumbu ya Mtakatifu Benedict mbele ya Majengo ya kanisa hilo
Sehemu ya Majengo ya Kanisa hilo ambapo pia kuna Hospitali kubwa.
Kiukweli eneo hili la Petamiho linapendeza sana na kuvutia.
Haya ni sehemu ya Makaburi ya watakatifu wa Kanisa hilo la Peramiho waliofariki miama mingi iliyopita,ambapo Baadhi ya waumini wa Kanisa hilo huwa wanafika na kuzuru makaburi hayo.
Jengo la Benki na ilipo Maktaba ya Vitabu
Sehemu ya Majengo yalipo makazi ya Mapadri na Madaktari.
Barabara ya Kuelekea Seminari Kuu,Peramiho.
Kanisa KATORIKI ni jipya duniani? Mimi najua kanisa KATOLIKI
ReplyDeleteAsante mdau kwa kutuweka tukio hili limenikumbusha mbali, mimi nilisoma Shule ya Sekondari ya wasichana ya Peramiho ambayo ilikuwa chini ya wabenedictine na baadhi ya walimu wetu walikuwa Masista. na hilo kanisa ndo tulikuwa tunasali na ilikuwa sehemu ya outing, hahahahahah
ReplyDeleteWe Misupu usipotoshe bana.
ReplyDeleteWakatoliki hawaiti USHARIKA bali wao wanaita PAROKIA ya....
Usipotoshe bana, kama hujui uliza bana uelekezwe bana!
Dah! hayo majengo ni legacy a mkoloni,mkoloni asingekaa hapo pasingekua hivyo. Siku hizi tuna wakoloni weusi..ni nomaa wanaiba bila kujua kesho itakua vipi.Kidumu chama cha Mapindizi!!
ReplyDeletekidumu...!!!.na udumu ukoloni mweusi
DeleteDuu hii imenikubusha mbali miaka ile ya 91 na 92 ambapo vijana wa songea boys waliwatosa ndugu zao tamsala Ila mimi nakumbuka jinsi sosage za ukweli za hapa zilipokuwa zinatengenezwa na mabruda na tofali za kuchoma ni kiboko tuwe tunaweka mara kwa mara vitu vyetu vizuri kwenye display sio tu issue mbaya na mataifa yaliyoendelea ni wajanja katika kuweka vivutio vyao na kuvitangaza zaidi na kuficha mabaya tuige mfano huo
ReplyDeleteAngejenga mjenzi wa leo angechakachua na kuripua kazi, tujifunze kutenda veme wajibu tunaopewa, itawezekana wabongo???. Siyo kila kitu kizuri afanye mzungu tu.
ReplyDeleteThank you soooo much misupu nimefurahi kuona Peramiho tena baada ya siku mingi, mtoto wangu wa pili alizaliwa hapo 1990! Natumaini Mheshimiwa Jenister Mhagama Mbunge atafurahi pia.
ReplyDeleteBro Michuzi,
ReplyDeleteUmenifurahisha uliponiambia makaburi ya watakatifu. Mtakatifu nani kazikwa hapo kwa mfano niambie? Hamna mtakatifu kazikwa hayo makaburi.
Ni mazuri na ni ukumbusho wa kitamaduni ila pia tuone jinsi yalivyo imara hadi leo. Tuombe tu mola wasiyachome moto!!!
ReplyDeleteAsante kaka Michuzi yaani leo umenikumbusha mbaliiii saana nilisoma Peramiho girls siku hizo palikuwa panaitwa (Vatican City) yaani tulipikwa ki maadili na kimasomo mpaka leo popote niendapo sina shida ya kuishi na jamii. Namkumbuka sister Martina,Fidelis, Goretha Edisa,Kesha, Mr and Mrs Zenda, Mr and Mrs Jacobo, Mr. msuya n.k God bless you all
ReplyDeleteimeingia kwenye ramani hiyo
ReplyDeleteYuko Mtakatifu mmoja anayetarajiwa kutangazwa anaitwa sister Bernadetha.
ReplyDelete