Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Fatuma Ally akizungumza machache wakati wa uzinduzi rasmi wa ufugaji wa kuku wa kibiashara kwa Chama kimoja cha ushirika Chenye wanachama wasiopungua mia mbili ambacho tayari kimeundwa na wakazi wa wilaya hiyo.
Baadhi ya Wadau wa Chama hicho wakifatilia maelezo wa Mkuu wa Wilaya
Na Abdulaziz Video,Chamwino.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Fatuma Ally amezindua rasmi ufugaji wa
kuku kibiashara wilayani humo kwa Chama kimoja cha ushirika Chenye
wanachama wasiopungua mia mbili ambacho tayari kimeundwa wilayani
humo.
Mkutano huo wa aina yake uliokutanisha baadhi ya
viongozi,Mabenki,NGOS,wakulima,wafugaji,Wenye maduka,mama Ntilie,Wenye
mabucha,wachuuza kuku,Wenye hoteli,Wenye mashine za kusaga na kukamua
mafuta na wataaalamu wa mifugo .
Mkutano huo uliokuwa katika sura yenye kuonyesha bayana dhana ya "
SMARTPARTNERSHIP ambapo Wananchi wa wilayani Chamwino mkoani Dodoma
wamehimizwa kuwekeza kwenye ufugaji kuku wa asili ili waweze
kukabilina na baa la njaa linalosababishwa na mabadiliko ya tabia ya
nchi.
Akifungua mkutano wa wadau wa ufugaji kuku wilayani humo,Mkuu wa
Wilaya hiyo Fatma Ally alisema ufugaji bora wa kuku wa asili unao
nafasi kubwa ya kukwamua jamii kiuchumi ambapo wananchi wa wilaya
hiyo kuweza kujiwezesha kujitosheleza kwa chakula kwa ufugaji kuku ili
kuziba pengo la ukame kwa kuwa wananchi wataweza kununua chakula cha
kutosha kwa mahitaji ya kaya zao.
“Wilaya yetu inakabiliwa na ukame ambao hata mtama hauwezi
kustawi…wananchi hawanabudi kuwekeza kwenye uzalishaji wa kuku ili
kipato kitokanacho na ufugaji huo kiweze kutumika kununua chakula ”
alisema Ally.
Aliongeza kuwa “Mkutano huu unalenga kuwaktanisha wazalishaji na
walaji ili kurahisisha masoko…ili kuhakikisha soko haliyumbishwi na
walanguzi tutaunda ushirika wa wafugaji kuku utakaosimamia soko hilo
katika wilaya yetu ”.
Awali mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Adrian Jungu
alisema tayari halmashauri yake imenunua majogoo 3400 wa kisasa na
wamegaiwa kwa wafugaji wilayani humo ili kurahisisha ufugaji sambamba
na ufugaji bora wa kuku wa asili.
“Hadi sasa wilaya inakadiriwa kuwa na kuku 350,000,tunaweza kuzalisha
zaidi na kuwa mkombozi wa kipato cha wananchi wetu ambao wanalazimika
kujitosheleza kwa chakula kutokana na ukame” alisema
Jungu na kufafanua kuwa
“Ili kurahisisha ufugaji huo, wananchi tunawahamasisha wajiunge kwenye
vikundi mbalimbali, viwepo vya utengenezaji chakula cha kuku,
kutotolesha vifaranga, kutibu magonjwa na vya masoko nasi kuwaunga
mkono.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...