Mkutano wa kumi na mbili wa Bunge utaanza siku ya Jumanne tarehe 27 Agosti, 2013 na kumalizika tarehe 13 Septemba, 2013. Mkutano huo unafuatia kumalizika kwa vikao vya wiki mbili za Kamati za Bunge kuanzia tarehe 12 Agosti, 2013.

Siku ya Jumatatu tarehe 26 Agosti, 2013 kitafanyika kiako cha kupeana maelezo (briefing) na baadae kufuatiwa na  Vikao vya Kamati za vyama vya siasa (Party Caucas) kuanzia saa kumi na moja jioni.

Katika mkutano huu Bunge linatarajia kujadili na kupitisha miswada sita kama ifuatavyo:

  1. Muswada wa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji wa Mwaka 2013 [The National Irrigation Bill, 2013].
  2. Muswada wa Sheria ya Takwimu wa  Mwaka 2013 [The Statistics Bill, 2013].
  3. Muswada wa Sheria ya Vyama vya Ushirika wa Mwaka 2013 [The Cooperative Societies Bill, 2013].
  4. Muswada wa Sheria ya Mfuko wa Akiba wa GEPF wa Mafao ya Wastaafu wa Mwaka 2013 [The GEPF Retirement Benefits Bill, 2013
  5. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013 [The Constitutional Review (Amendment) Bill, 2013.
  6. Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni wa Mwaka 2013 [The Referendum Bill, 2013].

Aidha, Bunge linatarajiwa kupitisha Azimio la kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Ushirikiano katika Masuala ya Ulinzi (The East African Protocol on Cooperation in Defence Affairs) na Kuzindua Taarifa ya Maendeleo ya Tanzania [Tanzania Human Development Report]. Ni katika kipindi hicho kutafanyika pia Semina Kuhusu Mradi wa Vijiji vya Milenia uliopo Uyui Mkoani Tabora.

Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
22 Agosti 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...