THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WADAU WA UTOAJI HAKI WA CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE NCHINI WAKUTANA KUJADILI UTOKOMEZAJI WA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA YANAYOAMBATANA NA RUSHWA YA NGONO

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA),mama Salma Kikwete (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono mara baada ya kukabidhiwa kitabu cha mwongozo wa namna ya kushughulikia mashauri mbalimbali ya kisheria alichokabidhiwa na Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania Mh. Jaji Engera Kileo leo jijini Dar es salaam.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete (kushoto) akizungumza jambo na Bi. Salome Anyoti Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Jinsia, Usawa na Uwezeshaji wa Wanawake leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono wakiwemo waheshimiwa Majaji wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa warsha hiyo ya siku 1.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) , mama Salma Kikwete (kulia) akiagana na viongozi wa Chama Cha Majaji Wanawake Tanzania mara baada ya kufungua wa warsha ya siku 1 ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono.
Washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono wakiwa katika picha ya pamoja na mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO


Kuna Maoni 2 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Jamani tuwe wakweli tu lakini Mama Salma anapendeza sana, seriously toka amekuwa first lady, sijawahi kuona picha hata moja amevaa vibaya, au marangi rangi ya ajabu. She knows how to dress from head to toe, mimi binafsi ninamsifu, na kumu admire and as a woman truly i feel so proud kuwa na first lady anayevutia na kupendeza namna hii; hongera mama Salma! Hope itakuwa ni mfano wa kuigwa kwa first ladies watakaofuata.

  2. Anonymous Anasema:

    Mdau wa Kwanza,

    Hata mimi nakuunga mkono kwa Kauli hiyo, pia ni muhimu akina mama hawa ambao ni mifano mizuri Mama Salma Kikwete, Mama Bilal Mama Pinda na wengineo wengi wawe wanaalikwa ktk Hafla za wasichana hasa hawa Ma-Miss ili angalau wasichana waone mifano mizuri na kujirekebisha!!!