WABUNGE WA MUUNGANO AMBAO WAKO ZIARANI UK WALIPATA FURSA YA KUTEMBELEA OFISI ZA WAZEE WA KAZI SERENGETI, KAMPUNI AMBAYO INAMILIKIWA NA WATANZANIA WAISHIO UK. PAMOJA NA MENGI WALIYOYAONA OFISINI HAPO, PIA WALIWEZA KUSHUDIA JINSI UKAGUZI WA MAGARI UNAVYOFANYIKA KWA KUTUMIA MASHINE ZA KISASA.
MSAFARA HUO WA WABUNGE KUMI ULIONGOZWA NA MHESHIMIWA HAMIS KIGWANGALLA AMBAYE MBUNGE WA NZEGA NA MWENYEKITI WA KAMATI YA SERIKALI ZA MITAA.
KATIKA TUKIO AMBALO LILIVUTIA WENGI NI PALE MBUNGE WA SERENGETI MHSEHIMIWA DR KEBWE ALIPOSEMA ANAJISIKIA YUKO JIMBONI KWAKE NA KUFURAHI SANA KUONA JINA LA SERENGETI LINAVUMA KILA KONA ZA UK. WABUNGE WALIFURAHISHWA KUONA JINSI VIJANA WA KITANZANIA WALIVYOWEZA KUJITENGENEZEA AJIRA WENYEWE WAKIWA UGENINI
Mbunge wa Serengeti akiwa na Wazee wa kazi
Wazee wa Kazi wakiwa na Mhe Hamisi Kigwangala
Waheshimiwa wakiangalia gari linavyokaguliwa kitaalamu kabla ya kusafirishwa kwenda Afrika Mashariki
Waheshimiwa wakiwa na Wazee wa Kazi
Waheshimiwa wakiangalia ukaguzi wa gari linalokaribia kusafirishwa kwenda Afrika Mashariki
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...