Wakili wa Zitto Kabwe akizungumza na wanahabari nje ya mahakama
Zitto Kabwe akipeana mikono na Wakili wa CHADEMA,Tundu Lisu baada ya kukibwaga chake chake.
 Wakili wa chama cha CHADEMA,Mh Tundu Lisu akizungumza na vyombo vya habari nje ya Mahakama kuu Kanda ya Dar Es Salam juu ya maamuzi yaliyotolewa na mahakama hiyo kuhusiana na kesi ya Zito Kabwe dhidi ya chama chake.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe amekibwaga chama chake,kufuatia  Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa, kuridhia zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya Chadema, hadi kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho itakapomalizika. Jaji huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza kusikilizwa Februari 13, mwaka huu.

Aidha Wakili wa chama cha CHADEMA,Tundu Lisu ameeleza kutoridhika na maamuziki ya Mahakama,hivyo akabanisha kuwa  Zitto Kabwe atabaki kuwa Mbunge wa Mahakama,na kama tujuavyo Mbunge wa Mahakama una  muda wake basi tujipe muda tuu..alibainisha Tundu Lisu.
 Tundu Lisu akiwatuliza na  kuwasihi wafuasi wa chama chake CHADEMA kutokufanya fujo na badala yake waondoke eneo hilo kwa utulivu na amani.Nje Mahakama makundi ya wafuasi wa CHADEMA na Zitto Kabwe walikuwa wakirushiana mawe kiasi hata mmoja wa wafuasi wa CHADEMA kujeruhiwa kichwani kwa jiwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Watanzania wengi bado hatujafamu maana ya siasa. Tunadhani kuwa siasa ni ugonvi, uadui, unyama, uhasama, vita, mapiganao, mauaji, matusi and things of that nature.

    ReplyDelete
  2. Kuna mihimili mikubwa mitatu ya dola, ambayo haiingiliani, ama sivyo? Nayo ni Bunge = (Kutunga Sheria); Executive (Utawala) = Utekelezaji; na Mahakama = Cha Mchanja Kuni.
    Mbona ya huyo Tundu Lissu yanaingiliana? M-Bunge wa Kutunga Sheria na mara wa Mahakamani kutekeleza cha Mchanja Kuni?
    Najua kuna wakati hata m-Bunge Nimrod Mkono wa Musoma Vijijini aliwahi kuwa wakili wa Executive wakati wa kesi ya maji nchini mbali ya kukimbia kutaka kumwakilisha Ditopile kwa tuhuma za uuaji na pia kukimbilia huko Amerika kutaka kumwakilisha Daudi Balali.
    Je, kuna vikonflikti vya interesti? Nifundisheni mnaojua zaidi! Na kama hujui, nyamaza ukae pamoja nami watufundishe.

    Usibane bwana ankali, la sivyo nitakunyima baadhi ya nyimbo uzipendazo!

    ReplyDelete
  3. Lisu kwa nini una tatizo na nchi kufuata sheria? Mbunge kisheria ni mbunge halali kuzidi wasio kisheria.

    ReplyDelete
  4. Zito alienda chuo cha kikwelii, sio vyo vya kata.

    ReplyDelete
  5. NAMPENDA SANA ZITO KABWE, YAANI UBARIKIWE SANA HUNA CHUKI NA MTU ANGEKUWA BUNDUKI HAPO ASINGESHIKANA MIKONO NA WEWE, LAKINI WEWE UMEMSHIKA LISU BIG UP, HERI WENYE KUUDHIWA KWA AJILI YA HAKI, MAANA HAO WATAUONA UFALME WA MUNGU. BARIKIWA SANA.

    ReplyDelete
  6. Tundu lissu kashindwa na wakili asiye na jina na mdogo.kumbe ni kelele tupu za Tundu lissu kujidai mwanasheria mahiri.hamna kitu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwee wewe ckui kama unaelewa unachokisema, em kumbuka kesi za maana na zenye mashiko alizozipangua lisu mf. Rufaa ya lema arusha na kurudishiwa ubunge wake, kesi ta lwakatare tena ya ugaidi bt aliishinda sembuse hii icyoata na mmashiko ya kuzuia kimjadili??? Just kumjadilo?? Mfyuu naamini ata nafc yako inakusuta kwa uliyoyaandika. Watanzani wasasa si wa miaka ileee ya 90's kweusi. Tunajielewankuliko unavyodhani. Na ni kwanini hataki kutoka chadema na anadai hakuna democrasia??? Y???? Aende bana

      Delete
  7. Wewe mdau hapo ndio hulijui ulisemalo...kesi zote hizo ulizotaja mwanasheria wa CHADEMA alikuwa dogo Alberto Msando na sio Tundu Lisu...huyu Tundu Lisu domo kaya tu huko Bungeni...kwa habari ya uanasheria na technicaliies hamna kitu...Jamani sio kila mwanasheria anaweza kuwakilisha mtu mahakamani...sheria ni technicalities sio u domo kaya....Yani unakuwa na hoja ambayo ina support ya sheria..hoja za Tundu Lissu zilikuwa hazina msingi wa kisheria na za kitoto kabisa..kwanza anaonekana hata utafiti wa kisheria hakufanya..mahakama sio lele mama Tundu Lissu...ona sasa ulivyoumbuka!..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...