Na Mashaka Mhando,TANGA 

VIKOSI vya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa,vinamshikilia Edwin John Mponji (31) kufuatia kwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga na kujitambulisha kwamba yeye ni koplo wa jeshi la Wananchi JWTZ akitaka kijana wake afanyiwe mpango wa kuingizwa Jeshi la kujenga Taifa.

 "Koplo" Mponji alikwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Halima Dendego Januari 16 mwaka huu siku ambayo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa ilikuwa katika zoezi la kuwafanyia usaili vijana wanaotakiwa kujiunga na jeshi la kujenga Taifa (JKT).

Akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mponji alijitambulisha kuwa yeye ni afisa wa JWTZ ambaye kwa sasa yupo kikosi cha 36 KJ Mkoani Pwani ambapo aliambatana na kijana Emmanuel Joseph akitaka afanyiwe mpango ili apate nafasi.

Hata hivyo wakati akitoa maelezo hayo,Mshauri wa Mgambo wa Wilaya ya Tanga,Sir Meja Albano Semfuko alimtilia shaka na kumjulisha Mkuu wa Wilaya ambaye aliamuru ashikiliwe kwa mahojiano zaidi. Akizungumza na waandishi wa habari,Mkuu wa Wilaya ya Tanga alisema baada ya mahojiano ilibainika kuwa Mponji sia askari wa JWTZ ndipo akalazimika kupelekwa nyumbani kwake mtaa wa Magomeni Jijini hapa alipopekuliwa alikutwa na sare za JWTZ zikiwa na cheo cha koplo.

Alisema wakati akikamatwa,Mponji alikuwa amevaa kaptura ya jeshi la Polisi lakini alipowekwa rumande ya kituo cha Polisi Chumbageni alifanya njama za kuivua na kisha kumpa mahabusu aliyekuwa akitoka ambaye alitoweka nayo.

Mponji alionyeshwa kwa waandishi wa habari akiwa amevalia sare ya jeshi la Wananchi ambapo alipohijiwa alishindwa kutoa maelezo ya kueleweka juu ya wapi alikokuwa amezipata sare hizo inagawa alikiri kuwa aliwahi kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kikosi cha 841 KJ Mafinga. 

Kufuatia tukio hilo,Mkuu wa Wilaya ya Tanga aliamuru Jeshi la Wananchi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kumfanyia uchunguzi wa kina ili kubaini mtandao wake.
'Koplo' feki wa JWTZ akiwa ofisini kwa mkuu wa wilya.
 'Koplo' feki akijiandaa kupanda  kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi
 'Koplo' feki akiwa na pamoja na Luteni Yahya Wangwe na Mteule daraja la pili Albano Semfuko

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

 1. Huyu jeshi feki anafanana na yule mdau wa kijiwe cha ughaibuni!!

  ReplyDelete
 2. The mdudu,mpeni kibano changuvu huyo ili kama kuna wengine kama yeye iwe fundisho tosha why alichezee jeshi letu tukufu la JWTZ linalo ogopeka africa yote kwa ushupavu wake,

  ReplyDelete
 3. Ni vema uchunguzi wa kina ufanyike kubaini hali halisi ya hicho kinchodhaniwa kuwa ni "utapeli" .... unaweza kubaini kumbe ilikuwa ni njaa tu .... apewe msaada ikiwa itabainika kuwa kilichomponza siyo uhalifu hasa bali ni njaa tu, mambo hayo huwa yanatokea...Lakini ikiwa kweli anayohistoria ya uhalifu huko nyuma, basi sheria ichukue mkondo maana kwa kweli hata kitendo cha kumiliki kombati za JW nadhani ni kosa (provided hizo kombati ni genuine, maana huwenda nazo zikawa feki)

  ReplyDelete
 4. Huyo atakuwa anakikosi cha utapeli ebu uchunguzi uwe wa kina ili kumbain vizuri zaidi asilitie doa jeshi letu linaloaminika kwa kila fani apelekwe lupango hafai kabisa huyo

  ReplyDelete
 5. Ajira tabu bongo sasa hiyo si ujasiliamali. Afadhali ana kibarua chake feki.

  ReplyDelete
 6. mpeni kazi huyu aende jeshini atakuwa askari bora!

  ReplyDelete
 7. Ugumu wa Maisha kipimo cha akili lakini sio kukurupukia Magwanda /Sare za Jeshi!

  Mfano anajipachika Ukoplo akiambiwa haya sasa moja kwa moja unatakiwa kuungana na Majeshi ya UN Brigade Tanzania Congo DRC utasema nini?

  Utadai unaharisha ama utasema nipeni ruhusa nikaage nyumambi na kupata fursa ya kukimbia?

  Kwenda Viani mchezo?

  ReplyDelete
 8. ''Mwanajeshi Feki'' Edwin John Mponji kazi anayo !

  Picha ya chini mmeona Luteni Yahaya Wangwe (mwenye shati la kijani lisilo na Kombati) anavyo mwangalia akijieleza Edwin?

  Hapo wakienda naye Kikosini atakesha usiku kucha akicheza Gwaride !!!

  ''Arooo Kopro Edwini si Mwanageshi weye kwa kuruka muguuu pande , moja mbili tatu moja''!!!

  ''Amuri moja, mbele tembeaaa'' (hapo amri ikitoka hata ukikutana na ukuta unatakiwa usipinde kona uendelee tu na mwendo wa gwaride)

  ReplyDelete
 9. Jamani isiwe tabu !

  Tupo ktk Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, wakati nchi jirani walikuwa wanakama waendesha Maboda boda wakidai wamekiuka taratibu za biashara na kuwaingiza Jeshini na kuwapa Mafunzo ya Uanajeshi.

  Jamaa suluhisho ni kuwa asiadhibiwe wala asichukuliwe hatua (tupo ktk Ushirikiano wa Afrika ya Mshariki tafadhali) ni kuwa moja kwa moja jamaa epelekwe kuongeza nguvu huko kwenye mahitaji makubwa ya askari Jeshi la Rwanda kwa KAGAME !

  ReplyDelete
 10. Kwa uelewa wangu wa Kusoma sura na Saikolojia jamaa sio bure!

  Usoni kwake Edwin John Mponji Askari Feki, ukimtazama anasomeka ya kuwa kama hatakuwa na Matatizo kidogo ya Akili, basi atakuwa ni ''mfuasi mzuri wa Bob Marley'' kwa kuwa pamja na kuwa yupo chini ya ulinzi wala hana wasiwasi wala tahamaki!

  Badala ya kumpeleka Lupango ya Kijeshi waanze kwa kumpima akili kwanza!!!

  ReplyDelete
 11. It was a joke, nothing serious let the young man go he did not steal anything mbona anasiasa wanatoa kazi kwa ndugu zao hamwakamati

  ReplyDelete
 12. Hahahahaha!

  Wajameni Bangi mbaya, naungana na Mdau wa 10 hapo juu, Bangi la Shambalai, Usambaani Tanga hilo.

  Jamaa ameyakanyaga amevutia sehemu yenye joto Tanga Mjini wakati Wafuasi wazuri wa MARLEY wanaujuw ukali wa mzigo huo wanavutia Vijijini hukohuko Milimani kwenye baridi.

  Jamaa anaonekana wazi ni Msela wa Maskani Ngamiani-Tanga pale karubu na Stendi kubwa ya Mabasi ya mikoani ni kuwa amezidiwa na Ganja (mzigo wa kutoka Shambalai Usambaani Milimani huko Lushoto-Tanga) hana Uwanajeshi wali nini tena inaonekana hata Uhalifu wenyewe asingeweza kuufanya kwa kuwa ni kama mtu asiye na kili timamu na asiyejua alifanyalo.

  ReplyDelete
 13. Hehehehehe Mdau wa 10!

  Hapa Tanzania mnamweka Edwin J. Mponji ktk Kundi la Wahalifu wakati huko nchini Rwanda kwa Kagame watampokea kwa Gwaride la Heshima na Ushujaa la Kijeshi kwa matarumbeta!

  Nadhani kwa tukio la makabidhiano haya wakifanya akina Afande LUTENI Yahaya Wangwe na Albano Semfuko inawezekana Mzozo baina ya Raisi Kikwete na Raisi Kagame utakwisha (TUTAKUWA TUMEISAIDIA RWANDA KIJESHI) na kwa nini Kagame KWA MSAADA NA USHIRIKIANO HUO WA MAJESHI asicheke kwa mara ya kwanza?

  ReplyDelete
 14. Mhhh, ni kweli Mdau wa 10.

  Uvutaji wa Bangi na ulaji wa Mirungi ukiitumia sana unaweza kuwa na ndoto za ALI NACHA na kujiona kana kwamba wewe ni Jenerali Mkubwa sana wa Majeshi!

  ReplyDelete
 15. Je, ''Kamanda Edwin J. Mponji'' na Kombati lako na Mbavu zako begani upo tayari kwenda Sudani Kusini?

  Hapo ulipo wewe ni 'Mizambwa Enterprises' yaani Feki in maana ukikubali kwenda ktk Operesheni Sudani Kusini vitani moja kwa moja utawekewwa CROWN katika kofia yako ambayo wewe huna (kwa kuwa wewe ni Mizambwa) na hapo hapo utakuwa Askari wa halali!!!

  ReplyDelete
 16. Ukiangalia kwa undani, yeye hana 'ndugu' wa kumsaidia kupeleka kimemo cha kuomba kijana aingizwe jeshi....akaona ajitoe ufahamu aende front mwenyewe....

  ReplyDelete
 17. Huyu jamaa si Mhalifu wala si Muasi bali ni BANGI na NJAA tu!

  Alikuwa anajaribu maisha kumtafutia kazi kijana wake hivyo kama baba ilimbidi awe jasiri ili kumnusuru mwanaye apate ajira.

  Mwacheni aende zake akalime!!!

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...