Ankal, 
mosi naomba nichukue wasaa huu kukushukuru kwa kazi nzuri ya kutuhabaraisha wana ughaibuni. Unatufikishia habari za nyumbani zinazotufariji tulio mbali na nyumbani. Ankal kabla kuendelea zaidi, napenda niseme machache ya moyoni kutokana na mada nzito ya juzi kutoka kwa kijana wetu mahiri john ,mashaka

naomba pia uniruhusu kusema machache kuhusu mwanazuoni John Mashaka kwa sababu ametugusa kwa mamilioni. na hapana shaka wasomaji wote wa hii blog watakubaliana na mimi kuhusiana na mada zake zinazoonyesha jinsi kijana huyu alivyo na, hekima, upeo na umahiri wa hali ya juu. hakuna swali tena kwamba ndugu mashaka anakubalika kuwa na busara na kipaji cha kipekee. ni mtu mwenye maono na nguvu ya ushawishi. nashawishika kusema kwamba, yeye ni lulu ya tanzania. Alizungumzia kwa ufasaha mkubwa haki zetu watanzania ughaibuni. amediriki kuzungumzia kwa ustadi mkubwa swala ambalo wengi tunaliogopa, ametusemea mamillioni na hatuna budi kumshukuru

kwa kifupi mimi ni mzaliwa wa Kagera. Nimesoma elimu ya sekondari na hata ya kati mkoa wa bukoba. baada ya elimu ya kati, nilijaribu sana kujiunga na chuo kikuu udsm , kusomea uandisi, licha ya kuwa na daraja la kwanza, sikufanikiwa. nilipangiwa kusomea uvetinary kitu ambacho sikupenda, basi nilikaa miaka miwili nikifanya vibarua vya ujenzi hadi mwaka1988. nilitamani sana kuendelea na masomo yangu. Scholarship nyingi zilitolewa na nchi za kigeni, marekani na uingereza, licha ya kuwa na qualifications za kutosha nilinyimwa ila divisheni 3 na hata 4 walipata udhamini katika mazingira tata. 

watu wasiokuwa na qualifications walipewa zile nafasi. basi na mimi kwa vile sikuwa na jina kubwa nyuma yangu sikufanikiwa , nilijitahidi kukusanya vijihela kidogo na hatimaye kuondoka nchini Tanzania kuelekea uturuki, ambako pia nilipigana miezi 5 kukusanya hela za kunifikisha urusi ambako nilitaabika sana kusoma. baada ya kulemewa nililazimika kutafuta uraia ili nipate msaada wa kielimu. Leo ni raia wa Urusi, nimesoma shaada ya kwanza,masters pamoja na phd kwa hela za warusi na kupata kazi Siberia, ambako nimeingia ubia na matajiri kuchimba mafuta. 

Hii inanirudisha kwenye mada ya ndugu Mashaka John. Nilichukua uraia wa urusi ili nipate elimu ambayo Tanzania haikuweza kunipa. Elimu ambayo ilitolewa kwa upendeleo. Leo nataka kurudi tanzania kama mzaliwa wa tanzania anayetambulika kikatiba, lakini kuna baadhi ya wanasiasa wanazuia hilo kutokea.

ninasema wazi kwamba natamani kurudi nchini tanzania na kuwekeza kwenye sekta ya gesi, au nirudi na wawekezaji ambao ntashirkiana nao, lakini nazuiliwa kwa sababu natambulika kama Mrusi.  Ninachosema kwa uwazi ni kwamba, kwa sasa niko tayari kutoa $2million kuwasaidia wagombea wote mkoani Bukoba watakaounga na kutetea haki zetu za kuzaliwa hata kama ni wapinzani. Sijui tafsiri hii itakuwaje lakini, haki yetu sasa lazima tuipiganie. Mimi ni raia wa kirusi kimakaratasi lakini moyoni ni raia wa tanzania

asanteni 
Mdau

E Rwezaura, Siberia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Ohhhhhhh no, unafanya nini yuko.

    ReplyDelete
  2. Hata viongozi wameshamsoma. John Mashaka ni jinias.jamaa kichwa hareeeeeeee

    ReplyDelete
  3. Basi, achia huo uraia wa kirusi, nenda ubalozini ukaombe kurudishiwa uraia wa kitanzania huku unarudisha passpoti yako ya Urusi kwa wao wenyewe, (kusema kweli, passpoti hio haikusaidii popote isipokua Urusi, afadhali ya Tanzania). Halafu rudi nyumbani kama unavotaka, na hao mainvestors, na elimu yako na pesa zako, kajenge nchi kama unavyotaka. Lakini najua, hutafanya kwa sababu, unataka kuishikilia hiyo passpoti ya Urusi, incase things get tough... 'when the rough gets going, the tough get going'. The solution is very easy, you want to go back home, go get your passport back and swear your loyalty to Tanzania and give up your Russian passport. Then I will believe your commitment.

    ReplyDelete
  4. Madispora acheni kupoteza muda wenu bureee!

    Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya Pasipoti moja tu (yaani hakuna Uraia Pacha.

    Hivyo kuupoteza Utanzania iwe kwa njia yeyote ile ama kutokufika Tanzania kwa zaidi ya mwaka kama zilivyo nchi zingine duniani (bila hata kuripoti ktk Ubalozi wa Tanzania uliopo karibu na wewe nje), mmekwisha vunja Sheria za Uraia za nchi.

    MSILETE VIGEZO VISIVYO KUWA NA MASHIKO KAMA HAKI YA KUZALIWA IWE KIGEZO CHA KUDAI URAIA PACHA, WAKATI MLIKWISHA VUNJA SHERIA ZA NCHI ZA URAIA NINYI WENYEWE.

    KUMBUKENI YA KUWA SHERIA NI MSUMENO NA KUWA KAMWE SHERIA HAINA LIKIZO!

    ReplyDelete
  5. Nyie mtatuletea shida tu; yaani mnataka kuja kuonyesha kuwa wote mliokimbilia huko mlipata mateso hapa nyumbani ndio mkakimbia? Sasa mnataka kurudi kufanya nini?

    ReplyDelete
  6. Hoja ya raia pacha ukiliunganisha na jina kama hili la ziwa Victoria basi inakubalika.

    ReplyDelete
  7. mdau wa urusi, kuna msemo unaweza kumtoa mhaya uhayana lakini tabia zake za kihaya kama aziwezi kuisha. majivuno kama kawaida, ndio una millioni mbili, mpaka useme? and of cousre
    of Tanzania new generation, john mashaka is the NEXT PRESIDENT. Huyu kijana asipokuwa kiongozi basi tanzania ni kichw acha mwenda wazimu
    wasipomchagua mashaka president 2020 NAENDA CHADEMA KUTOKA CCM

    ReplyDelete
  8. Weka picha ya huko Siberia ili tuamini hizi sensational stories kabla hatujaingia kujadili mada tata ya uraia pacha.

    Huko Siberia umepata utaalamu wa kuchimba mafuta? na Je, Tanzania unataka kuja kuchimba mafuta, almasi n.k kama huko Siberia au utakuwa kazi yako kubwa 'kuunganisha Ma-Oligarchy-wa-Kirusi kuja wekeza Tanzania.

    Mbili wanadiaspora sasa hivi tunawajadili mpata vyeti/kitambulisho cha unasaba na Tanzania hivyo hutalipa viza kuigia Tz, pia utakuwa na fursa kibao kama kumiliki ardhi, uwekezaji n.k je hiyo haitoshi unataka uraia pacha tu?!

    Mdau
    Team Pasipoti Moja Tu

    ReplyDelete
  9. Hiyo $2,000,000 afadhali ununue nyumba za NHC au uwekeze kwenye biashara ya hisa, SACCO yenye faida kuliko kuziweka kwenye siasa. Waache wanasiasa wachakarike kama wengine.

    ReplyDelete
  10. Mmh mbona ni kama inatangazwa rushwa hapa

    ReplyDelete
  11. Jamani wabongo hatuna shukrani, ukisema umefanya au utafanya hiki au kile, jamaa watasema unajionyesha. Kwa mfano ndugu Rwezaura hapa. Lakini hapo hapo wanapenda kuuliza diaspora mmefanya nini?!(Kama ni wajibu wetu pekee kuijenga TZ) Hapa nadhani kuna mtu mmoja(wachache) anaeipinga uraia pacha, yeye kazi yake kuandika maoni kibao ili ionekane kuna watu wengi kumbe ni mmoja tu. Michuzi naomba ufuatile anwani ya IP, hapa wanajifanya wako wengi kumbe si kweli, kwani mawazo ni yale yale ya chuki na wivu usio na msingi.Fuatilia, ikitoka tu habari ya uraia pacha basi yeye na maoni kibao wakati mmoja.

    ReplyDelete
  12. Uraia pacha ama preferential uraia kwa nchi fulani tu; ikiwa ni pamoja na watoto wa mabalozi waliobakia ughaibuni?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...