Ankal akijiandaa kuingia ndani ya ndege yake ndogo inayoweza kutua popote aliyoinunua hivi karibuni kutoka katika visiwa vya Ushelisheli (Seychelles Islands) ili kuepukana na adha ya foleni jijini Dar es salaam. 
Ankal ameiambia Globu ya Jamii kwamba amekuwa akisomea urubani wa ndege hiyo kwa siri kwa mwaka mmoja na sasa ameshatimiza  masaa 450 hewani na tayari ameshapata leseni ya kupaa katika jiji la Dar (mchana tu, kati ya saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni) na kutua katika viwanja mbalimbali vikiwemo vya Gymkhana (kwa wilaya ya Ilala), Uwanja wa Taifa wa zamani (wilaya ya Temeke) na Biafra (wilaya ya Kinondoni) na Maisara (Unguja). 
Maombi yake ya kutua katika miji  mingine mikubwa kama vile Mbeya, Mwanza, Arusha, Rukwa, Katavi, Njombe, Dodoma na Morogoro yanashughulikiwa na huenda akafanikiwa mara baada ya sehemu za kutua katika mikoa hiyo zitapothibitishwa na mamlaka husika.
Ankal anakuwa blogger wa kwanza Mtanzania mwenye kumiliki ndege yake mwenyewe. Anasema hiyo ni hatua moja kubwa aliyokuwa akiiota miaka kadhaa wakati alipokuwa anafikiria si tu namna ya kupambana na foleni mijini, bali pia kufikia habari moto na kwa muda muafaka..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 84 mpaka sasa

 1. Haaaa haaaa tumestuka LEO NI SIKU YA WAJINGA, hakamatiki mtu hapa!

  ReplyDelete
 2. Siku ya wajinga hiyo ha ha ha ha najua unawezo Ankal wangu lakini aaaaahhh...!! umetupiga changa la macho.

  ReplyDelete
 3. April's Fool>>> hehehee

  ReplyDelete
 4. Hongera sana Ankal. Mungu ni muweza wa yote kwake yeye aaminiye na kumtukuza. Mimi binafsi nimefurahishwa na hatua hii nzuri uliyoipiga kwani naamini itarahisisha kazi yako kwa kiasi kikubwa nasi tutafaidika pia.

  ReplyDelete
 5. April Fools Day....

  ReplyDelete
 6. SIKU YA WAJINGA DUNIANI. HONGERA KWA NDOTO NJEMA

  ReplyDelete
 7. Hahahaha ankal hongera sana kwa kupiga hatua kubwa Kama hiyo kwenye karne hii yenye changamoto nyingi kwa sie wabeba boksi, swali la kizushi mbona hii sehemu Kama pale uwanja wa nanihiu pembeni mwa jnia maana hizo rangi za jengo na Ac za sanyo zilizochoka malaya Kwikwi Kama hapa ni sychells as u said... jibu tafadhali na kumradhi Kama kwa mbaaaali ntakuwa nimekutibulia kwa bbys maana uzee umeisha kule kwenye kampeni so unajua tena bbys za mujini ukiwa na ka private jet tena mweh kwa ubuah..ni hayo tu

  ReplyDelete
 8. tehe tehe tehe......fools day

  ReplyDelete
 9. Siku ya wajinga ankal!! But was good one though!

  ReplyDelete
 10. Hongera sana Ankal na MUNGU akuzidishie am really proudly of you

  ReplyDelete
 11. Ankal,

  Hongera na pia sikukuu ya wajinga!

  ReplyDelete
 12. Karibu kwenye ulimwengu wa kupasua anga.... angalia jamaa wa TRA wasikupe usajili wa MH370

  Karibu Aprli 01

  ReplyDelete
 13. Wajinga Day Ankal

  ReplyDelete
 14. hongera sana kama kweli...ila nawasiwasiiiiiiii

  ReplyDelete
 15. tarehe moja mwezi wa nne,

  ReplyDelete
 16. Mjinga mwenyewe

  ReplyDelete
 17. Asante ankal.. Tunajua hii ni April Fools day.. Lakini kwa uhakika imekaa vizuri hii, fanya kweli basi.

  ReplyDelete
 18. siku ya wajinga

  ReplyDelete
 19. april fool!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 20. Ankal safari hii hutu pati ;) 1/04 / 2014; )

  ReplyDelete
 21. I'm not fool. Hahaaa

  ReplyDelete
 22. 'You can fool people some time but you can't fool people all the time'.

  Don't try to hoodwink peole please

  Nimekuona eeeeee. April fool!

  ReplyDelete
 23. siku ya wajinga leo

  ReplyDelete
 24. Duh! Big up ankal. ...Hongera sana kaka!

  ReplyDelete
 25. Hongera, ha ha ha
  Nionavyo mimi ingekuwa bora kama ungejinunulia helichopa.

  ReplyDelete
 26. April wise men's day.
  Hahhaaaaaaaaa hutupati ng'o

  ReplyDelete
 27. Ankal kweli kaukata siyo mwenzetu tutakuwa tunamuona kwa juu lakini atatua wapi akiwa anaenda kwao kwani kuna uwanja wa ndege. Au ndiyo April fool.

  ReplyDelete
 28. Hahahaha. Ankal ungenunua kwanza fulana zingine kabla ya hiyo ndege.

  ReplyDelete
 29. Hongera sana uncally wetu kwa kununua ndege kwa ajili ya april/1 tu, kwani kesho hutakuwa nayo

  ReplyDelete
 30. Congratulations, big up, hongera sana, kila la kheri, Tegeta utatua kwenye uwanja gani, nataka niwe nawahi lift nitachangia wese.

  ReplyDelete
 31. Hongera Ankal (KAMA NI KWELI!!!)

  ReplyDelete
 32. siku ya wajinga duniani

  ReplyDelete
 33. Congratulations Ankal. Ila tu taarifa hizi zilipaswa kutufikia jana au kesho na sio leo kwakuwa leo ni tarehe 01/04/2014. Kwa wajanja mmeshaelewa ninachomaanisha.

  ReplyDelete
 34. Ankal na vijijini pia kuna shemu kuna viwanja.Omba pia kutuwa katika kiwanja cha kijiji kiitwacho TUTAYAONA kilichopo mpakani baina ya kijiji cha Kufikirika na Kusadikika katika wilaya ya Mambousiayaige.

  ReplyDelete
 35. JINGA`S Day

  ReplyDelete
 36. Anko hampati mtu, n'a April fool

  ReplyDelete
 37. hahaha anko asante kwa April full...

  ReplyDelete
 38. Is it April Fools day au nimekosea?

  ReplyDelete
 39. well done uncle happy fools day

  ReplyDelete
 40. APRIL FOOLS DAY!

  ReplyDelete
 41. Tumekushtukia Anakali, yaani hapa humpati mtu. Tarehe 1 Aprili hiyo.

  ReplyDelete
 42. Ni tarehe 1/4 so ankal kajipange upya!

  ReplyDelete
 43. Hongera sana Michuzi kwa hatua hiyo,Sasa ni News kwa kwenda mbele.

  ReplyDelete
 44. April Fools hiyo!

  ReplyDelete
 45. Hongera uncle kwa wazo zuri isije kuwa ni foolish day. Nachelea kuamini.

  ReplyDelete
 46. Sikukuu ya wajinga ....

  ReplyDelete
 47. shauri yanko ankali si uwezi wa kukutafuta DEEP SEA hatuna.

  ReplyDelete
 48. we ankal unafikiri hatujui kwamba leo ni siku ya wajinga

  ReplyDelete
 49. Ze Mamba:
  Kwi kwi kwi. Haya ankal, kanyaboya zuri sana, na nimelipenda. Umewapata wangapi? Kwi kwi kwi.

  On a serious note, inabidi ununue ndege ankal, maana wewe ni alwatani kwenye hili gemu.

  ReplyDelete
 50. Sikukuu ya wajinga leo.

  ReplyDelete
 51. Kaka nashukuru kwa kutukamata vizuri siku ya wajinga nami nimekuwa mjinga kwa leo asante sana mkuu wa kazi.
  Ila kwakuwa umenikamata vizuri nakuombea ununue helkopta kabisa ili kukidhi matakwa yetu sie wapenzi wa mi-newzzzzz ya kukata na shoka.

  ReplyDelete
 52. Ndio Mzee wa Libeneke! Napenda kutoa Pongezi kwa Jitihada zako na mafanikio ya kuliendeleza Libeneke! Pia Hongeza sana kwa Kumnunua huyo ndege ingawa inatia mashaka kuona ndege hana Jina! Ndio maana hisia zangu zinaniambia kuwa ni Jiwe la Fool's Day so Ngastuka Mzee! Nice try though! Ila kama ni kweli Hongera tena Uncle!

  ReplyDelete
 53. Uncle hili ni changa la macho sikukuu ya wajinga leo ,mdau wa Ukerewe

  ReplyDelete
 54. Braza michu acha hizo leo sikukuu ya wajinga

  ReplyDelete
 55. 1.4.2014

  ReplyDelete
 56. umeniokota kweli siku ya wajinga leo.du...

  ReplyDelete
 57. Hichi ni kibonzo cha Fulls Day! Good luck with that!

  ReplyDelete
 58. 1st April ni siku ya akina nani vile?

  ReplyDelete
 59. NADHANI LEO NI TRH 1

  ReplyDelete
 60. Sikukuu ya wajinga

  ReplyDelete
 61. Hapo kama Dar sa Salaam terminal 1 vile???.....hahahahaha.....April 1st

  ReplyDelete
 62. Hongera, weka nembo ya Fulanaz basi.

  ReplyDelete
 63. Hongera Ankal...lakini kununua hako kapipa siku ya April 1st mimi bado hujanipata.

  ReplyDelete
 64. April fool!!!! Misupu nimekushtukia....ha ha ha

  ReplyDelete
 65. "Fools Day 01 April ni Siku ya wajinga"

  Ankal kwa leo sitokupa Hongera
  labda kama ukitoa hizi habari tena
  kesho nitakupa hongera saana mkuu

  Mikidadi- Denmark

  ReplyDelete
 66. 1st april Ankal teh teh teh

  ReplyDelete
 67. Its april fooooool

  ReplyDelete
 68. Kama nakumbuka vyema tarehe kama hii mwaka fulani huko nyuma ankal aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya, sasa kanunua ndege, mhhh, mambo yake si mabaya!!!

  ReplyDelete
 69. Ndege hii inafafa ya kwangu niliyopaki mujini Dar es salaam. Imepata pancha ya tairi la kulia.

  Hongera sana

  Karibu kilabuni ankal

  pilot mzoefu

  ReplyDelete
 70. Leo si ile siku yao....!

  ReplyDelete
 71. April moja utawapata wengi ankal! lol!

  ReplyDelete
 72. Wooote nyie mmechemsha leo sio siku ya wajinga but the Mduduz day.

  ReplyDelete
 73. ukiwa mjinga...na sisi sio wajinga..

  ReplyDelete
 74. Ama kweli Fools Day! Ndege gani kutua uwanja wa biafra ambapo pamekuwa dimbwi la maji!!

  ReplyDelete
 75. kwa april2nd..... mimi nitanunua ikulu ndogo pale chamwino ankal, sitaki tena kukaa darchalama, kuna vumbi na fujo nyingi mno....ankal

  ReplyDelete
 76. Hakikisha unaisadili kwa number AK040114.

  ReplyDelete
 77. DUUH BRO HONGERA SANA ILE AHADI YAKO IME TIMIA KAMA TULIVYO ONGEA USUBIRI MPAKA SIKU KAMA YA LEO U BREAK NEWS NA KWELI USEMI WAKO WATU WATAFIKIRI APRIL CHANGA LA MACHO INA BIDI KUWAPA KIZARAMO KALAGA BAHO BIG UP BRO

  ReplyDelete
 78. Angalia usipotelee mto ruvu au wami kama malysia airline = april fool

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...