MAMA mzazi wa mmiliki wa mtandao wa Saluti5, Said Mode - Bi Desta Mohamed - amefariki ghafla Jumatatu ya tarehe 31/3/2014 saa 1 za jioni.

 Alipata homa kali Jumapili mchana, akapelekwa hospitali (IMTU) akapata matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Hali yake haikuwa mbaya wala ya kutia mashaka.

 Jumatatu akaamka vizuri na akashinda vizuri hadi saa 12 za jioni hali ipoanza kubadilika tena. Akafariki akiwa njiani kupelekwa hospitali. Msiba uko Dar es Salaam, Mbezi Beach Old Bagamoyo Road kituo cha Zena Kawawa.

Mazishi yatafanyika Jumanne 1/4/2014 saa 10 alasiri kwenye makaburi ya Mbezi Beach (New Bagamoyo Road) mbele kidogo ya  Masana Hospital.
INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RRAAJIUN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. "Inna Lillahi Wainna Ilayhi Rajiun". Mola mpokee mja wako, mughufirie dhambize, mnusuru na adhabuzo zote za dunia na akhera, umpumzishe palipo pema peponi na kesho awe ni miongoni mwa waja wako wema watakaoingia katika yako 'Jannatu N'naaem' . - AMEEN.

    Na tuwe pole ndugu, jamaa na marafiki wote wa Marehemu Bi Desta Mohamed.

    ReplyDelete
  2. Bwana alitoa.....bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Poleni wafiwa na Mwenyezi Mungu awepe nguvu, faraja na kumbukumbu njema za Mama. Amen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...