Na Mwandishi Maalum 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ametoa shukrani na pongezi za pekee kwa kuwa moja ya nchi 29 kati ya 193 ambazo hadi kufikia Mei Sita mwaka huu, zilikuwa zimelipia kwa ukamilifu na kwa wakati michango yake katika Umoja wa Mataifa. 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kati ya nchi hizi ambazo katibu Mkuu amezipongeza. Tanzania imelipa zaidi ya dola za kimarekani 450,000 kama sehemu ya michango yake kwa Chombo hicho cha Kimataifa. 
Na kwa miaka mitano mfulululizo imekuwa ikilipa kwa wakati na kwa ukamilifu. 
Kwa Tanzania kulipitia michango siyo tu kwamba, ni kielelezo cha uwajibikaji kama nchi mwanachama, lakini pia ni utekelezaji wa utawala bora na ni heshma kwa taifa mbele ya Jumuiya ya Kimataifa. 
Pongezi za Ban ki Moon kwa nchi hizo zimo katika taarifa yake kuhusu hali Fedha katika Umoja wa Mataifa. 
Taarifa hiyo iliyowasilishwa na kisha kujadiliwa na Wajumbe wa Kamati ya Tano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya Utawala na Bajeti ya Umoja wa Mataifa. Katibu Mkuu amezitaka nchi nyingine kuiga mfano wa nchi hizo kwa kile alichosema hali nzuri ya fedha ya Taasisi hiyo ya Kimataifa pamoja na uendeshaji wa shughuli zake, unategemea sana michango ya wanachama wake, michango inayotakiwa kutolewa kwa wakati na kwa ukamilifu. 
Kila nchi mwanachama hutakiwa kulipa kiasi cha michango katika bajeti za Umoja wa Mataifa kutokana na uwiano wa uchumi wake katika dunia kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Umoja wa Mataifa. Bajeti za Umoja wa Mataifa kwa mwaka ni zaidi ya bilioni 10 zikijumuisha bajeti ya Kawaida, bajeti za misheni za kulinda Amani na mahakama za kimataifa za makosa ya Jinai. Pia kuna bajeti za miradi maalum kama ukarabati wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kiasi cha dola 2 bilioni kwa mradi wote. 
Nchi nyingine ambazo zimekwisha kulipia michango yake ni Australia, Austria, Brunei Darussalam Canada, Denmark, Equatorial Guinea, Finland, Hungary, Germany, Iceland, Israel, Japan, Latvia, Liechtenstein na Netherlands Nyingine ni New Zealand, Norway, Samoa, Senegal, Singapore, Sweden, Switzerland, Timor-Lester, Turkmenistan, , Georgia, Kenya na Jamhuri ya Korea.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Ban Ki Moon

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...