Na Andrew Chale
TAASISI ya  Mwangaza wa buradani Zanzibar  (Zanzibar Light Entertainment ) ya mjini Unguja,  Zanzibar, kupitia vyombo vya habari, imemtangaza rasmi , Raisi mstaafu wa  Chama cha Soka  Zanzibar, (Zanzibar Football Association-ZFA) Mzee Ally Fereji Tamim  kuwa mgeni rasmi kwenye michuano maalum ya soka la ufukweni  lijulikanayo kama  (Zanzibar Beach Soccer Championship Bonanza) linalotarajiwa kufanyika Agosti  Mbili mwaka huu katika fukwe za  Nungwi.
Kwa mujibu wa taarifa yao hiyo  kwa vyombo vya habari, ilieleza kuwa, michuano hiyo ya Zanzibar Beach Soccer inatarajiwa kuzikutanisha timu mbalimbali za Visiwani humo, Bara na nje ya Tanzania ambapo watakutana kwa pamoja na kushiriki kichuano hiyo maalum, kwenye fukwe hizo za Nungwi.
Mwandaaji wa michezo hiyo, Muslim Nassor ‘Jazzphaa’  alisema  wamejisikia furaha kwa viongozi wa juu na wadau wa soka kuwaunga mkono, kwani inatia moyo katika kuendesha shughuli za kimichezo kama hizo. “Tunapongeza wadau wote, kikubwa  zaidi, ni Mzee wetu,  Ally Fereji Tamim kukubari  kuwa mgeni rasmi, pia milango ipo wazi kwa wadau wengine kujitokeza katika kufanikisha zaidi tukio hili ,muhimu” alisema Muslim  Nassoro ‘Jazzphaa’.
Aidha, aliendelea kuwaomba  mashirika, makampuni, taasisi za Serikali na za watu binafsi na wadau kujitokeza kwa wingi kudhamini Bonanza hilo la  Zanzibaar Beach Soccer, ilikufikia malengo yaliyokusudiwa katika kuifikia jamii na kuiweka pamoja.
Muslim  Nassoro ‘Jazzphaa’ aliongeza kuwa, Michezo hiyo yenye lengo ya kuweka watu pamoja, kudumisha utamaduni na kuhimalisha afya ya mwili, pia itakuwa na burudani mbalimbali. Lakini pia alitoa shukrani za dhati kwa uongozi wa beach soccer na kamati yote kwa ujumla katika kufanikisha jambo hilo.
Kwa upande wake, Rais wa beach Soccer Zanzibar,  Bwana Ally Sheikh Alhabshy  alipongeza Taasisi hiyo kuandaa michuano hiyo ambapo amesisitiza kuwa Wadhamini wasisitite kutoa udhamini wao na kuja kuona mchezo huo unavyochezwa.
Zanzibar Beach soccer Bonanza kwa  mwaka huu itakuwa ni ya mara ya tatu, kwa taasisi hiyo kuandaa michezo hiyo ya soka la ufukweni.
Michezo hiyo ya soka la ufukweni imekuwa maalufu katika nchi mbalimbali zenye fukwe, ambapo wananchi na wageni kutoka mataifa mengine ujumuika kwa pamoja.
Kwa mwaka huu pia kutakuwa na burudani kali na ya aina yake itayaoporomoshwa na dj mkali anayetikisa visiwani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...