Leo Waziri wa Ujenai Dkt. John Pombe Magufuli kama ilivyokuwa kwa  amesisitiza Makandarasi wanaojenga barabara za kwenda Liganga kwenye makaa ya mawe zikamilike ndani ya muda uliopangwa na kuheshimu matakwa ya Mkataba na kwamba kusiwepo na kisingizio cha kuwa wao ni wakandarasi wazalendo. 
Alisisitiza barabara hizo zinatakiwa zikamilike mapema tayari kwa kupitisha mitambo yenye uzito wa tani 150 itayaosafirishwa kwenda Liganga. 
 Aidha, Dkt.Magufuli akiongea na Wafanyakazi wa TANROADS, TEMESA na TBA wote wa Mkoa wa Njombe alimhakikishia Kaimu RAS wa Mkoa wa Njombe kuwa serikali kupitia Wizara ya Ujenzi mwaka wa fedha 2014/2015 imetenga kiasi cha shilingi bilioni 28 kutoka mfuko wa barabara ambapo shilingi bilioni 17 zitatumika kwenye barabara kuu na za mikoa na shilingi bilioni 11 ni kwa ajili ya kuhudumia barabara zilizo chini ya Halimashauri. 
 Dkt.Magufuli amewahakikishia wananchi wa Njombe ya kuwa mwaka huu wa fedha 2014/2015 serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuanza kuzijenga barabara za Njombe kwenda Makete yenye urefu wa kilomita 109.4 na ile ya Itoni kwenda Manda yenye urefu wa kilomita 211 kwa kuanzia kila barabara zitajengwa kwa kiwango cha lami kilomita 50.
Dkt.Magufuli,Dkt.Wanyancha (M/Kiti Mfuko wa Barabara), Kaimu RAS Njombe,Wafanyakazi wa TANROADS,TEMESA na TBA wote kutoka Mkoa wa Njombe walipokutana kwenye kikao na Waziri wa Ujenzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2014

    Ujenzi wa reli ndiyo endelevu kwa kubebe mitambo hiyo ya tani 150 kwa ajili ya ujenzi wa mgodi.

    Pia reli inafaa kubebe mali itakayo zalishwa na mgodimara uzalishaji utapoanza bila kusahau wadau wengine wa pembezoni mwa reli.

    Mdau
    Vision 2025

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...