Mwanahabari wa Reuters nchini Bw. Fumbuka Ng’wanakilala (aliyebeba msalaba), pamoja na wadogo zake, Lugendo  (kushoto) na Manyanda (kulia), wakiwaongoza waombolezaji waliobeba jeneza lenye mwili wa Baba yao, Marehemu Mwl. Nkwabi Ng’wanakilala baada ya kuwasili nyumbani kwao Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Julai 01 mwaka huu, kwa ajili mazishi. 
Mwl. Ng’wanakilala, ambaye alikuwa Mhadhiri katika Idara ya Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), jijini Mwanza alifariki Juni 27, katika Hospitali ya Bugando baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo na tumbo. PICHA ZOTE/JOHN BADI
Mzee Nkwabi Ng'wanakilala enzi za uhai wake.
Ndugu, jamaa na waombolezaji wakilitelemsha jeneza lenye mwili wa Mwl. Ng’wanakilala kutoka kwenye gari baada ya kuwasili nyumbani Kibamba.
Sehemu ya waombolezaji wakiwa msibani Kibamba.
Mkurugenzi Msaidizi  wa Idara ya Habari MAELEZO  BW. Raphael Hokororo  (kati) akiwa na wadau wa habari waliokuwepo mazishini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...