Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.

"Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine".

Baada ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali ya kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio na hivyo yeye mwenyewe sasa anatakiwa aende akaripoti haraka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam bila kukosa.

Ni muhimu sana kwa Askofu Josephat Gwajima kuripoti yeye mwenyewe badala ya Kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake katika jamii.

Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.

Imetolewa na: 
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Binafsi nilifedheheshwa na kusikitishwa sana kwa matusi mazito aliyokuwa akiyaporomosha huyu mchunga kondoo. Hili jambo halikubaliki hata kidogo hatakama mchungaji Gwajima hakufurahia tamko la askofu Pengo.Ilibidi awe muungwana ikizingatiwa yeye ni kiongozi mkubwa wa kanisa lake hilo la kiroho. Hamna mwenye mamlaka ya kutukana mtu hata kama amekuudhi hupaswi kumtukana mtu. Kitendo cha askofu Gwajima kumtukana kardinali Pengo inabidi kilaaniwe na kila mtu anaye mfata mungu kwa unyenyekevu. Hivi tujiulize hii jeuri ya huyu mchungaji Gwajima kumtukana kiongozi mkubwa kama Kardinali Pengo anaitoa wapi? tunaomba mamlaka husika vyombo vyote vya usalama kumchukulia hatua kali huyu Askofu ili iwe fundisho kwa viongozi wengine wa kiroho wanao tumia madhabau kukashifu na kutukana watu wengine. Tunaomba Jeshi la polisi nchi pasipo kupapasa macho wamchukulie hatua kali huyu mchungaji Gwajima maana amemdhalilisha Baba Askofu Mwadhama Kardinali Pengo. Mungu ibariki Tanzania iwe nchi ya aman, amina.

    ReplyDelete
  2. matusi hayakubaliki katika jamii kama kuna ukweli katika matamshi yake hayo yanakubalika sasa isiwe kazi ya kuchagua matusi peke yake sidhani kama askofu Gwajima ameamka tu na kuanza kazi ya kumtukana kadinali pengo kama vile hana ibada ya kuongoza kwa siku hiyo.
    jeshi la polisi angalieni na muyachuje matusi mbali na kama kuna ukweli wowote ndani ya matusi basi ukweli huo nao uwekwe wazi halafu kesi ya shambulio la matusi inaweza kuendelea peke yake.kiini cha matusi kifahamike ili kosa lisirudiwe na kama hakuna sababu pia tufahamishwe.hawa wote ni viongozi wa kanisa hakuna malaika au mtume hapo.

    asante.

    mwanakondoo wa mungu.

    ReplyDelete
  3. Gwajima amejibu kile ambacho kimetafsiriwa kwamba amemtusi Pengo si sawa bali amemkemea Askofu Pengo kama Askofu mwenzake na sio kumtusi na kuelezea kuhusu taarifa ambayo imetapakaa kwenye mitandao ya jamii kwamba anatafutwa na Polisi msikilize hapa Askofu Josephat Gwajima phD hapa

    https://soundcloud.com/ufufuo-na-uzima/taarifa-ya-askofu-dr-gwajima-kuhusu-kuitwa-na-polisi-kujieleza-27032015

    ReplyDelete
  4. Serikali pls kuweni makini na maamuzi ya ili jambo na tungependa msiwaachie Polisi pekee kufanya maamuzi yoyote yale na Wanasheria wa Serikali wenye uzoefu mkubwa muweze kuwasaidia Polisi.

    Mimi binafsi ni Mkristo tena Roman Catholic lakini hapa sifungamani mahali popote, Huyu bwana Gwajima ana wafuasi wake walio wengi sana na Mh Pengo ana wafuasi wake wengi sana ila ningemuomba Mh Rais na Wazee wengine wengi wa nchi hii wenye busara mfanye maamuzi yaliyo mazuri kwa nchi yetu ili kesho na kesho kutwa haya mambo yasitokee tena ningependa Muwakutanishe hawa watu na waondoe tofauti zao maana itakuwa ni mara ya kwanza watu wa dini kutokwa na roho mtakatifu na kuamua kuchukua jaziba na kuhusisha Polisi badala ya kuwa kama Yesu aliyesema atakae kupiga shavu la kushoto basi mpatie shavu lingine na kusamehe. HAPA NIMESHANGAZWA KUONA HEKIMA YA BIBLIA NA MAANDIKO IMEWEKWA PEMBENI.

    Wazee wote wenye busara wa Kanisa na Maaskofu ndani ya nchi hii ninawaomba muingilie kati ili swala na ningewaomba muwaombe Polisi kusitisha maamuzi yoyote kabla hamjakimbilia haya mambo mngewaomba hawa wazee wawasaidie ili kuondoa hii tofauti iliyopo.

    Kwa Kuenzi misingi ya nchi hii kwa jinsi ilivyoundwa ningeshauri pia hii nchi ibaki kama ilivyokuwa mwanzo isifungamane ktk dini yoyote na isiwe na dini. Tusikubari ata siku moja Siasa za aina yoyote ikatufanya tuweke dini ktk nchi hii yetu nzuri tuliyorithi kwa Wazee wetu. Wewe mwanasiasa eidha wa dini yoyote Usikubari kutupeleka pabaya kwa kuwa wewe ni dini gani au eidha unategemea nafasi gani kisiasa. Wazee wangu wote walio ndani ya Usalama wa Taifa ningependa na ningeomba mfanye analysis nzuri kuhusu ili swala na maswala hayo ya Mahakama ya kadhi na kuishauri Serikali na sio kwamba nachukua ndugu zangu Waislam hapana kabisa tena Mke wangu ni Muislam na mmoja ya watoto wangu ameoa Muislam hivyo sina tatizo na hawa ndugu zangu bali nisingependa Taifa ili liwe na udini wowote ule ili watoto wetu wabaki kuwa na amani kama tuliyorithi sisi toka kwa Mababu zetu na kubaki kuoana na kusaidiana na kuwa wamoja! Nashangaa leo hii Taifa ili eti linataka kuwa na dini, linataka kuwa na makabila! hivi sisi ni akina nani haswa?! Kama wasingekuwa wakoloni wazungu na waarab kuja hivi sisi tungejua ukristo na uislam??! Basi nawaomba wenye maamuzi eidha Wabunge, Mawaziri, Mkuu wa nchi ndani ya nchi yetu ibaki kuwa bila dini na daima Tanzania itabaki kuwa Taifa Kubwa na lenye Amani hapa duniani. Mkumbuekeni Baba wa Taifa na Maono yake.

    Nimechukua muda wangu na kutumia haki yangu ya demokrasia kuzungumzia yaliyomo moyoni mwangu kwa Manufaa ya Taifa ili na watoto wetu na Kizazi kijacho.

    Mungu ibari Tanzania, Mungu Ibariki Afrika na Mungu Wabariki Mh Pengo na Mh Gwajima ili warudi makanisani na sio kubaki Polisi na Mahakamani.

    ReplyDelete
  5. Wanaoona kuwa alimtusi ni watu wa chini ila yeye alitumia lugha kwa mtu aliye sawa na yeye kihadhi, nafasi na utendaji. A language used between equals, maana wote ni maaskofu na viogozi.
    Tuwaachie watengeneze, tusiingilie.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...