Waziri wa mambo
ya Ndani ya nchi, Mathias Chikawe akizungumza na waandishi wa Habari ( hawapo pichani) kuhusiana na Taasisi za Dini na vikundi mbalimbali kuepuka kushiriki katika
vitendo ambavyo vinaashilia kuvuruga amani na utulivu nchini jijini Dar leo.
Baadhi
ya Waandishi habari waliohudhuria katika mkutano wa wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es salaam leo.Picha Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.
Na Chalila
Kibuda,Globu ya Jamii.
ASASI za Kiraia zilizosajiliwa chini ya Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi,vinavyojihusisha na siasa na kuacha katiba zao vitaanza kufutwa
kuanzia Aprili 30 mwaka huu.
Hayo
ameyasema Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mathias Chikawe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea
katika Kura ya maoni pamoja na Uchaguzi Mkuu,Chikawe amesema serikali iko imara
katika kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani hivyo watu wanaotaka kuharibu
amani kutumia asasi za kiraia na kuacha
katiba zao watafutwa.
Chikawe
amesema katika kuelekea uchaguzi kumekuwa na asasi za kiraia zikijihusisha na siasa kwa kuchangisha fedha
kwa ajili kuwashawishi viongozi wa siasa wagombee hiyo ni kwenda kinyume na
katiba zao na kutakiwa kufutiwa usajili.
Amesema
katika suala la ugaidi ni tatizo la dunia hivyo kinachofanyika ni kuimarisha
ulinzi katika maeneo yetu na kupata taarifa kwa watu wanaoingia nchini na watu
wanaobainika kutoa kuwa na taarifa wanawarudisha katika nchi zao.
Chikawe
amesema vijana wa kitanzania ambao wamekamatwa nchini Kenya kuhusika na ugaidi
hawana taarifa, wanachokifanya ni kupata taarifa kutoka Kenya kama kuna watu
wengine wapo katika kundi la al-shabab.
Aidha
amesema jeshi liko imara hivyo wananchi waishi kwa amani kwani serikali ina imarisha
ulinzi kuhakikisha amani inakuwepo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...