Waziri
wa mali asili na utalii, Lazaro Nyarandu akiwa na waumini mbalimbali baada ya
Ibada ya jumapili Jijini Arusha katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mjini
Kati ambapo Waziri Nyarandu alitumia nafasi hiyo kutangaza rasmi siku
atakayochukua fomu ya kuwania nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya
kuwania Urais kupitia chama cha Mpindunzi .
Waziri
wa maliasili na utalii, Lazaro Nyarandu akibadilishana mawazo na Kada wa chama
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, James Ole Milya baada ya ibada ya
jumapili iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Diyosisi ya mjini kati Arusha
ambapo Nyarandu alitumia nafasi hiyo kutaja rasmi kuwa tarehe 6 mwezi ujao
atachukua fomu ya kuwania nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM
kuwania urais .
**************
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,
Lazoro Nyalandu ambaye alishatangaza nia ya kukiomba chama Chake cha Mapinduzi
(CCM) kumteua kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, anataraji
kuchukua fomu ya kutimiza adhma yake hiyo Juni 7 mwaka huu mjini Dodoma.
ametangaza rasmi kuchukua fomu ya
kuwania nafasi hiyo baada ya kutangaza nia yake majuma kadhaa yaliyopita mkoani Singida.
Nyalandu anaungana na makada
wengine wa CCM kuingia katika kinyang’anyiro hicho ambapo anasema mpango na
dhamira yake ya kuwania kuteuliwa na chama chake uko palepale huku akijinasibu
kuwa dunia itaandika historia pale atakapo ibuka kidedea kwa kupeperusha
bendera ya ccm katika kinyang’anyiro hicho.
“Mpango na dhamira yangu ya kuomba ridhaa ya
Chama changu kuniteua kugombea urais mwaka huu upo palepale na dunia itaandika
historia pale nitakapo ibuka kidedea na kuipeperusha bendera ya CCM katika
uchaguzi wa mwaka huu,” alisema Nyalandu.
Waziri Nyalandu ataungana na
makada na Mawaziri wakongwe katika siasa za Tanzania katika kuwania nafasi hiyo
ndani ya CCM kama akina Edward Lowassa, Steven Wasira, Bernard Membe, Samuel
Sitta, na wengineo wengi ambao tayari wameshatangaza nia na dhamira yao ya
kuutaka urais.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...