THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

CHAMA CHA WANAWAKE WANASHERIA TANZANIA(TAWLA) WAFUTURU NA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA MWANA VINGUNGUTI JIJINI DAR.

 Watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam wakiwa wamekaa katika kituo hicho mara baada ya Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA),kuwatembelea na kufuturu pamoja nao katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Wanachama wa  Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) wakichukua Futari kwaajili ya kuwagawia watoto wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam jana.
Mfanyakazi wa Wanachama wa Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA),akiwawekea Futari kwaajili ya kufutari pamoja na watoto wa kituo cha watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo vingunguti jijini Dar es Salaam jana.
 Watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini wakifutari pamoja na wanachama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) walipo futuru pamoja na watoto hao katika kituo cha Mwana jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kituo cha watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, Mohamed Wage akiwashukuru wanachama wa Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA),walipoamua kutembelea kituo cha mwana.
Mwakilishi wa chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) akimkabidhi vitu mbalimbali Mkurugenzi wa Kituo cha watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, Mohamed Wage, Mara baada ya Kufutari pamoja na watoto hao.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.