Mkurugenzi wa The African Enterprise Challenge Fund (AECF), Hugh Scott akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na uzinduzi wa awamu ya nne ya dirisha la ufadhili wa kilimo cha biashara maalum kwaajili ya watanzania hapa nchini.
Afisa mkuu wa usimamizi, Sam Ng'ang'a akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkurugenzi wa The African Enterprise Challenge Fund (AECF), Hugh Scott.
Mkurugenzi wa kampuni ya Internation Tan Feed LTD, Faustine Lekule akizungumza na waandishi wa habari leo kwa jinsi kampuni yake ilivyoweza kunufaika na ruzuku inayotolewa na AECF kwa kuweza kugundua aina mbalimbalimbali za vyakula vya mifugo hapa nchini.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
MFUKO wa The African Enterprise Challenge Fund (AECF) umezindua awamu ya nne ya dirisha  la ufadhili wa kilimo cha Biashara na huduma za kifedha vijijini hapa nchini.

Ameyasema hayo Mkurugenzi wa mfuko wa The African Enterprise Challenge Fund (AECF), Hugh Scott wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Scott amesema kuwa sambambamba na kuzindua awamu ya nne kutakuwa na shindano lenye lengo la kuhamasisha watu wenye mawazo ya kilimobiashara kwaajili ya kupewa ufadhili wa waombaji watakaoshinda katika shindano hilo.

"Waombaji watakaoshinda watapewa ruzuku na mikopo isiyo na riba kati la dola za kimarekani laki moja na dola za kimarekani milioni moja", alisema Scott

Pia Scott ametoa wito kwa makampuni mbalimbali, sekta mbalimbali au vikundi yenye mawazo ya kilimobiashara kutuma maombi kwenye mtandao wa intaneti wa www.aecfafrica.org  ili kuweza kuomba  na kushindania shindano.

Aidha  Scott amesema kuwa shindano hilo lipo wazi kwa makampuni yanayotengeneza faida na linahamasisha makampuni ya ndani na kampuni ya kigeni kuomba nafasi hiyo lakini mawazo yake yawe ya kilimobiashara yatakayopendekezwa katika uombaji lazima yawe yanafanyika hapa nchini.

Pia amesema kuwa shindano hili limeshaanza kuanzia leo na mwisho wa kutuma maombi ni Disemba 15 mwaka huu.

Scott alitoa wito kwa sekta binafsi kuchangamkia frusa iliyotolewa na mfuko wa AECF  hapa nchini kutokana na kuzinduliwa kwa mara ya nne na kwa ufadhili wa kilimo biashara ili waweze kuitikia na kuwa na mawazo ya biashara yenye ubunifu ambayo yataleta manufaa kwa maisha ya watanzania waishio vijijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...