Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye ni mlezi wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi nje ya chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya kuhusu kifo cha utata cha aliyekuwa Katibu wa chama hicho Tanzania, Rashid Saleh kilichotokea hivi karibuni pamoja na ratiba ya mazishi yake yatakayofanyika jijini Mwanza.
 Marehemu, Rashid Saleh
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye ni mlezi wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADU), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Pubrishers LTD, Eric Shigongo (katikati), na wadau wengine kuhusu taratibu za mazishi za katibu huyo.
 Mjumbe wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Stanley Kilave (kulia), akizungumza na Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Clement Masanja (kushoto), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Pubrishers LTD, Eric Shigongo (katikati), wakati wa taratibu za mazishi zikifanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam leo.

 Msemaji wa familia ya marehemu, Jonas Marinyizu (katikati), akitoa shukurani kwa DC Makonda na wadau wengine kwa kuwezesha msiba huo pamoja na utaratibu wa mazishi utakavyo kuwa.

Mwenyekiti wa Chama hicho, Shaban Mdemu akizungumza katika mkutano na wanahabari

Na Dotto Mwaibale
MWILI wa Katibu Mkuu na Msemaji wa Chama Cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Rashid Saleh umesafirishwa jana kwenda kijijini kwao Kayenze wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa maziko.
Marehemu Saleh alifariki jana Novemba 21 Majira ya saa 8 mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wakati akipata matibabu ya maradhi ya figo ili kuokoa maisha yake baada ya kile kinachodaiwa kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni mlezi wa chama hicho, Paul Makonda alisema kuwa wamepata pigo kutokana na umuhimu na umahiri ambao alikuwa nao marehemu hasa katika kutetea haki za madereva wenzake sanjari na kuibua mambo mbalimbali ambayo yatabaki kuwa historia na kumbukumbu kwao.
"Saleh alifariki jana (Novemba 21) baada ya kusikia anaumwa ambapo hali yake haikuwa nzuri na madaktari walishauri nimlete Muhimbili kwa matibabu zaidi ambapo nilimfikisha lakini baada ya muda mfupi wakati madaktari wanahangaika kumtibu na kuokoa maisha yake alifariki,"alisema.
Alisema marehemu amekiacha chama sehemu ya mafanikio makubwa zaidi ya mabadiliko na mikataba ya haki za madereva nchi nzima huku akibainisha mazingira ya kifo na kutaka uchunguzi zaidi ili kujiridhisha na kifo chake uliofanywa chini ya uangalizi wa polisi.
"Hatukuona kama kuna haja ya kumuhifadhi mwili wa ndugu yetu hadi hapo tutakapojua nini chanzo cha kifo chake kwani majibu ndiyo yatatupa picha ya ugonjwa kwani tumehangaika tangu alipokuwa hospitali ya Kairuki ambapo tulipofika hapa ikabainika kuwa figo zake zote mbili hazifanyi kazi,"alisema.
Aliongeza kuwa marehemu alipelekwa hospitalini hapo kwa kitengo maalum huku akibainisha endapo figo zinashindwa kufanya kazi mzunguko mzima wa damu mwilini nao husimama ambapo madaktari walishirikiana lakini hawakuweza kuokoa maisha yake.
Mwenyekiti wa Chama hicho, Shaban Mdemu alisema kuwa msiba huo umewasikitisha sana kutokana na mazingira ya kifo chake huku akiitaka mamlaka husika kulisimamia suala hilo la kupatika kwa majibu sahihi juu ya kifo chake.
"Tunataka uchunguzi ufanyike na majibu yatoke yakiwa sahihi na yanayoridhisha juu ya kifo chake kwani amekufa na madai ambayo yapo ndani yao, hivyo serikali itambue kifo cha Saleh ni katika harakati za kudai haki ambayo tuliyawasilisha mbele ya aliyekuwa waziri mkuu Mizengo Pinda,"alisema. 
Alisema Saleh ni kiongozi wa taifa zima hivyo alimtaka rais Magufuli kuingilia kati suala hilo kwani kutokana na hali hiyo watamaliza wafanyakazi wote kwa kuwauwa katika mazingira kama hayo sambamba na kutenga siku rasmi kwa ajili ya maombezo ya msemaji huyo.
Harakati za kudai haki ya madereva
Marehemu Saleh alizaliwa mwaka 1966 Mwanza, ambapo hadi anafariki alikuwa katika harakati za kudai na kutetea haki za madereva ambapo Oktoba 2, mwaka huu alikaririwa akisema wamechoshwa na yanayoendelea kufanywa na Mamlaka ya Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (Sumatra) na Wizara ya Kazi na Ajira kuhusu kufumbia macho kero zinazoitatiza sekta ya usafirishaji hasa kwa madereva wa mabasi ya abiria na magari ya mizigo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...