Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu (katikati), akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shs. milioni 255 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kituo cha mawasilianio ya Jeshi la Polisi. Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Siro, Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi, Omary Issa (wa pili kulia) na kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka.
(Picha na Francis Dande)
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
 Baadhi ya wageni waalikwa.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Na Glory Chacky.
BENKI ya CRDB imekabidhi msaada wa sh. Milioni 255 kwa Jeshi la polisi kwa ajili ya  ujenzi wa kituo cha mawasiliano.

Akizungumza jana jijini Dar es salaam wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei amesema kuwa wanatambua kuwa jeshi la polisi ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi linahitaji mfumo bora wa mawasiliano kati yake na raia.

Alisema wameamua kuelekeza msada huo kwa jeshi la polisi kwa kutambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na jeshi hilo ya kuhakusha kwamba kuna usalama na amani kwa raia.

Kimei alisema juhudi za wanachi katika kujikwamua  katika umaskini  hazitafanikiwa kama kutakuwa na ukosefu wa usalama wa raia na  mali zao kwa ujumla.

Naye mkuu wa Jeshi la polisi IGP, Ernest Mangu alisema  kuwa wanashukuru kwa msaada huo kwani itasaudia kupunguza matukio ya kiualifu.

“ Kituo  hiki kitasaidia kulisogeza jeshi la polisi karibu zaidi na wananchi na kushirikiana nao katika kutaarifiana juu ya maswala ya kiualifu pindi yanapojitokeza”alisema Mangu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...