Kamishna wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya, akipunga mkono kwa baadhi ya wanahabari waliokuwepo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam leo, mara baada ya kusikilizwa kwa kesi inayowakabili yeye na wenzake wawili ambao ni waliokuwa Maafisa Waandamizi wa Benki ya Stanibic Tanzania, Shose Sinare pamoja na Sioi Solomoni waliofikishwa kwenye mahakama hiyo kwa makosa manane likiwamo la kutakatisha fedha kiasi cha Dola milioni sita za Marekani.
Kesi hiyo imesikilizwa tena leo Mahakamani hapo, ambapo baada ya kusikilizwa kwa muda wa takribani masaa matatu, kesi hiyo imeahirishwa mpaka Aprili 22 itakapotajwa tena na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande kwa kile ambacho Mahakama imeeleza kuwa mashtaka yao hayana dhamana.
Mmoja wa watuhumiwa katika kesi ya kutakatisha fedha kiasi cha Dola milioni sita za Marekani, Shose Sinare akisindikizwa na Askari wa Jeshi la Magereza kwenda kwenye gari Karandinga, tayari kwa safari ya kurudishwa rumande baada ya kesi yao kusogezwa mbele.
Sioi Solomoni akijiangaa kupanga Gari hilo.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imepuuza ombi la dhamana ya kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni ambapo wamerejeshwa rumande.

Kitillya, aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi Solomoni, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.

Dhamana yao imesikilizwa mbele ya Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu ambapo mawakili wa pande zote mbili waliwasilisha hoja zao.
Dk. Lingo Tenga ndiye aliyeongoza jopo la mawakili upande wa watetezi ambapo upande wa serikali umesimamiwa na Oswadi Tibabyekonya, Wakili Mkuu wa Serikali Mahakama ya Kisutu.

Upande wa utetezi uliomba mahakama kubatilisha mashitaka ya utakatishaji pesa haramu uliosababisha watuhumiwa hao kukosa dhamana. Tibabyekonya ameieleza mahakama kuwa, shitaka la utakatishaji fedha halina dhamana.

Upande wa utetezi ulifanya mapitio ya kesi mbalimbali zinazofanana na kesi hizo ikiwemo kesi namba 314 ya mwaka 2015 kwenye Mahakama ya Rufaa ya Mwanza iliyokuwa ikimkabili Kigunda Francis aliyeshitakiwa kwa kosa kama hilo lakini alipewa dhamana.

Christopher Msigwa, wakili wa serikali amesema kuwa kesi hiyo haina dhamana kwa sababu, kosa hilo linaathiri uchumi wa taifa.

Washitakiwa wamekosa dhamana na wamerudishwa rumande hadi tarehe 22 Aprili mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mbona uchunguzi ulishafanywa kule Uingereza na hukumu kwa upande wao ulishatoka? Kuna uchunguzi gani tena? Hii kesi imekwisha, wahukumiwe na warudishe walichochukua ili maisha mengine yaendelee.

    ReplyDelete
  2. Hatutashangaa wakiukumiwa kifungo cha miaka 3 watatumikia miaka 2 ndani mwaka 1 kufagia sokoni mchezo umekwisha,Lakini vibaka wezi wa simu miaka 30 jela

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...