Naomba unirishie taarifa yangu hii ili iweze kuwafikia wahusika waweze kuchukua hatua stahiki. Kuna uharibifu mkubwa sana wa mazingira unaondelea katika bonde la mto Mpiji huko maeneo ya Bunju na Mbweni Mpiji Manispaa ya Kinondoni. 

Malori ya mchanga yanasomba mchanga katika Bonde la mto Mpiji na kuziweka nyumba za wakazi jirani na Bonde hili kuwa hatarini na kukumbwa na mafuriko kutokana na mmonyonyo wa udongo na upanuzi wa bonde la mto Mpiji. 

Taarifa hii ilisharipotiwa kwenye vyombo husika kama NEMC na Police, lakini cha ajabu hali hii ya uharibifu inaendelea ili hali vyombo vya udhiti vipo lakini havitekelezi majukumu yao ipasavyo. Tunamwomba Mheshimiwa Raisi John Pombe Magufuli atumbue haya majipu ya taasisi husika kabla wananchi wake hatujafikwa na majanga.

Wasaalm,

Mdau Mkazi wa Bunju

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...