Mzunguko (Roundabout) na Stesheni kuu ya reli Kigoma. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said) 

NA K-VIS MEDIA

MKOA wa Kigoma umekaukiwa na sukari kuanzania Ijumaa Mei 20, 2016 na taarifa ya Ofisi ya Biashara ya Mkoa, imesema, Wakazi wa Manispaa ya Kigoma –Ujiji wavumilie hadi mwisho wa mwezi huu wa Mei.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mkoani humo, kabla ya siku ya Ijumaa, sukari iliuzwa kwa bei ya shilingi elfu 5,000 kwa kilo, kwenye eneo la Manispaa ya Kigoma-Ujiji, lakini Ijumaa maeneo yote ya manispaa hiyo hayakuwa na sukari hata hiyo ya shilingi elfu 5.

Akizungumzia uhaba huo mkubwa wa sukari mkoani humo, Afisa biashara wa mkoa wa Kigoma Deogratius Sanga, amekiri kuwepo kwa uhaba huo na kuwataka wananchi wa Manispaa hiyo kwua wavumilivu wakati serikali ya mkoa inatafutia ufumbuzi tatizo hilo. “Taarifa toka bodi ya sukari ni kwamba ile sukari iliyoahidiwa na waziri mkuu itafika mwisho wa mwezi huu, na tunategemea kuanzia mwezi ujao tatizo hili litakwisha”.alisema Sanga.
Sehemu ya Uwanja wa Ndege wa Kigoma.
Bandari ya Kigoma.
Mwalo wa Kibirizi.
Manispaa ya Kigoma- Ujiji
Uwanja wa Lake Tanganyika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2016

    Sehemu nyingine za Kigoma nzuri zingine kama Kibirizi sijui mipango miji walikuwa wapi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2016

    Poleni kwa upungufu ndugu zetu
    Jamaa umenifurahisha sana na picha hizi.Nitawaonyesha wajukuu kuwa hapo ndipo nilipoanza shule kwa white fathers kabla ya kuhamia Kasulu.Nakumbuka miye na wakorofi wenzangu tukienda kucheza kando ya ziwa hapo Kibirizi, kisha tukakoma maana mtu mmoja alikamatwa na mamba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...