1. Waarabu wamempachika Ngamia Jina la Meli ya Jangwani ('Ship of The DESERT) Kutokana na Uwezo Mkubwa alionao wa kustahimili shuruba za nyikani katika hari zote. Kwa Miongo kadhaa inamuwia vigumu sana kumuelezea Ngamia kwa kinagaubaga kutokana na mavumbuzi yanayogundulika kila siku kwa mnyama huyu. Hawa wanapatikana kwa aina mbili wenye Nundu moja na wenye nundu mbili (tazama picha)
2. Ngamia ana uwezo wa Kuishi Mwezi Mzima Bila Kula Wala Kunywa Huku Akiwa Amejitwisha Uzito wa Kilo Hadi Kati ya 200 na 500 Sawa na Magunia 5 yenye uzito wa kilo 100

2. Ngami Ndilo Tumaini Pekee la Usafiri wa Nyikani akiwa na uwezo wa Kutembea hadi Kilomita 50 kwa siku bila kula wala kunywa chochote

3. Wengi Hudhani Ngamia anahifadhi maji kwenye nundu, la hasha, Ngamia Hutumia Nundu Kuhifadhi Mafuta ambayo humsaidia nyakati za ukame wa chakula na maji,

4. Kwa Miongo Kadhaa, Ngamia Wametumika sana kwenye vita vya nyikani kutokana na umahiri wao wa kukabili michanga na huweza na kasi ya pekee mchangani kwani wana uwezo wa kukimbia km 48/saa, kifupi huyaweza hayo kutokana na kua na tabaka mbili za kwato zinazomsaidia asititie mchangani

4. Ngamia pia ana kope nzito kubaliana na mchanga wa nyikani

5. Ngamia anapodhoofika hutumika pia kama kitoweo na maziwa yake yana virutubisho maradufu ya vile vinavyopatikana kwenye maziwa ya Ng'ombe

6. licha ya Ngami Kufugwa kwa minajili  kwa kubeba watu na mizigo. Nywele zao pia ni aina ya sufu inayotumiwa kutengenezea mashuka, viatu mabegi, mahema na pia vitambaa vya nguo. Na bidhaa itokanayo na manyoya ya Ngamia huuzwa ghali sana kutokana na uimara wake
7. Ngamia ana uwezo wa kunywa galoni 40 kwa mkupuo mmoja na mkojo wa Ngamia pia hutumika kama mafuta (fuel) yasemekana pia mkojo wa ngamia na maziwa ya ngamia ni dawa inayotibu homa na unaweza kuwa hadi asilimia 80 ya visababishi vya saratani iliyo mwilini (Camel Urine caused the death of 80% in different cancer cells, including breast also camel urine reduced lung cancer cells to 84.75% and 92.81%,)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...