Mwanamuziki nyota wa miondoko ya Rhumba kutoka Jamhiri y Kidemokrasia Congo (DRC), Antoine Christophe Agbepa Mumba maarufu kama Koffi Olomide hivi majuzi alizikonga nyoyo za mashabiki wake wakati alipoitwa jukwaani na Mwanamuziki wake wa zamani, Fally Ipupa katika moja ya maonyesho yake aliyoyafanya huko Brazzaville ikiwa ni tamasha lake la kwanza tangu alipokumbwa na 'sakata la teke' nchini Kenya na kumsababishia kuswekwa jela kwa siku kadhaa.

Katika tamasha hilo, Kofii Olomide aliweza pia kusambaza video ya sehemu ya shoo yake hiyo aliyoifanya mjini Brazzaville.

Baada ya sakaka la teke nchini Kenya, Olomide alisafirishwa usiku wa siku ya tukio kwenda mjini Kinshasa DRC kutoka jijini Nairobi kufuatia kuenea kwa picha za video kwenye mitandaoni ya kijamii ikimuonyesha Mwanamuziki huyo akimshambulia kwa teke zito, Mwanamuziki wake wa kike wakati walipotua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi nchini Kenya.
Olomide alitoka kwa kupewa dhamana kufuatia shinikizo la mashabiki wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...