Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya jana walitayarisha hafla fupi kumuaga Mhe. Balozi John Michael Haule, ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria. Mhe. Haule aliteuliwa kuwa Balozi mwaka mmoja uliopita baada ya kutumikia Wizara ya Mambo ya Nje kwa miaka minne kama Katibu Mkuu.

Katika risala yao, watumishi wa Ubalozi walimuelezea kama 'mjenzi' aliyeimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Kenya, na kiongozi mtaalamu, mnyenyekevu na mwadilifu.

Mwakilishi wa Watanzania waishio Kenya, Bw. Victor Matemba, alimsifu Mhe. Haule kwa ari na juhudi alizofanya kufufua umoja wao ambao umedorora kwa muda mrefu. Ubalozi unaratibu uandishi wa Katiba mpya ya Umoja huo ambayo iko katika hatua za mwisho.

"Unaondoka wakati ambao ulezi na uongozi wako tunauhitaji zaidi. Tutakumiss sana Mheshimiwa," alisema Bw. Matemba. Akiongea kwenye hafla hiyo, Mhe. Haule alisema uhusiano kati ya Tanzania na Kenya ni imara, kinyume na taarifa za baadhi ya vyombo vya habari zinazodai kuwa kuna msuguano. "Uhusiano wetu ni mzuri sana."

Balozi alielezea wasiwasi kuhusu mtafaruku wa kisiasa nchini Sudan Kusini na kutaka hatua madhubuti zichukuliwe kuepusha mapigano zaidi, ambayo alisema yataathiri pia Watanzania waishio nchini humo.

Mhe. Haule, ambaye aliambatana na mkewe Mary kwenye hafla hiyo ya kumuaga iliyofanyika kwenye ofisi za Ubalozi, aliwashukuru watumishi wote kwa ushirikiano mkubwa waliompatia.
Mhe. Haule akiongea wakati wa hafla ya kumuaga jana. Kushoto ni mkewe Mary.
Mhe. Balozi Haule (aliyeketi katikati) katika picha ya pamoja na Maofisa Ubalozi. Kushoto ni Mama Mary Haule na Kulia ni Mkuu wa Utawala Ubalozini, Bi. Talha Waziri.
Mhe. Haule na mkewe katika picha ya pamoja na watumishi wa Ubalozi wanaotoka Kenya (Local staff).
Mwakilishi wa Watanzania waishio Kenya, Bw. Victor Matemba akitoa salamu zao kwa Mhe. Haule.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...