Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Selemani Mponda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kabla ya hafla fupi ya kusherekea miaka 19 ya benki hiyo na kuzindua wa huduma tatu za benki hiyo. Kutoka kushoto ni  Mkuu wa wa Kitengo cha Hatari David Lusala, kulia ni Mkuu wa Rasilimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga.
Meneja Operesheni wa Benki ya Exim, Manfredy Kayala akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Kadi za malipo za Exim (TANAPA cards, Master cards and VISA cards) ambazo zinaweza kutumika katika Hifadhi zote za Taifa chini ya TANAPA. Kadi hizi zitaboresha huduma ya malipo ya kielektroniki na pia kuzuia upotevu wa mapato katika tasnia ya Utalii. jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Raslimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga.
 Mkuu wa Kitengo cha hatari wa Benki ya Exim, David Lusala (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Selemani Mponda na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha uhasibu, George Binde.
Mkuu wa Raslimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga akionesha bango la huduma ya  Mfumo wa kujifunza kupitia mtandao unaoitwa Elimika ambao utaongeza uwezeshaji wa wafanyakazi kwa kiasi kikubwa jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...