THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DORIS MOLLEL FOUNDATION YATOA VITABU MASHULENI JIJINI DAR

August 9 ya kila mwaka, dunia huadhimisha Siku ya Usomaji Vitabu Kwa kila rika (International Book Lovers Day). Katika kusheherekea siku hiyo hapa nchini, Taasisi ya Doris Mollel chini ya Mwanzilishi wake, Bi. Dorice Mollel ilipata wasaa wa kutoa vitabu kwa shule tatu za jijini Dar es Salaam ambazo ni Shule za Sekondari za Tegeta na Mtakuja, pamoja na shule ya msingi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Vitabu hivyo vilitolewa kwa ufadhili wa Rehema Trust Foundation kwenda kwa Doris Mollel Foundation.

Tegeta Sekondari ilipata vitabu ishirini na mbili (22), Mtakuja Sekondari ilipata vitabu kumi na tisa (19) na shule ya msingi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilipatiwa vitabu nane (8),  pamoja na kuwashirikisha wanafunzi hao kati michezo iliyotolewa kwa ufadhili wa Turkish Airways ili kusaidia watoto wapende michezo na kuchangamsha ufahamu wao.
Mwakilishi wa Taasisi ya Doris Mollel, Edward Allan akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Tegeta kuhusu umuhimu ya kusoma vitabu vya kiada, mara baada ya kukabidhi vitabu hivyo.
Mwakilishi wa Taasisi ya Doris Mollel, Edward Allan akiwaonyesha kitu wanafunzi wa shule ya Sekondari Tegeta kwenye moja ya vitabu vilivyotolewa kwao.
Mwakilishi wa Taasisi ya Doris Mollel, Jerome Calvin (kulia) akimkabidhi vitabu Mmoja wa Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mtakuja.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwalimu J.k Nyerere wakicheza na kufurahia mchezo wa chase uliotolewa na Taasisi ya Doris Mollel.