Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) akiwa pamoja na wadau wengine wa Mahakama ya Tanzania walipotembelea kuangalia Maandalizi ya Jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililopo kwenye Shule ya Sheria Sinza leo jijini Dar es salaam. Baadhi ya Wadau wa Mahakama waliotembelea Mahakama hiyo ni Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mawasiliano, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (kulia) akiwaelezea jambo baadhi ya Makatibu Wakuu na watendaji wakuu wa Wizara na Taasisi za Serikali ambao ni Wadau wa Mahakama ya Tanzania walipotembelea kuona maendeleo ya Maandalizi ya Jengo litakalotumika kuwa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Sinza jijini Dar es salaam. Anayetazamana na Kattanga ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome na anayefuatia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Bibi Maimuna Tarishi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (kulia) wakiwaonyesha jambo wadau wengine wa Mahakama walipotembelea jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo jijini Dar esa salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (Kushoto) na Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Bibi Maimuna Tarishi wakizungumza jambo walipotembelea kuona maendeleo ya Maandalizi ya uanzishwaji wa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Sinza jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...