Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na
sehemu ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na
wakandarasi wanaosimamia miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) mara baada ya kuwasili wilayani Handeni mkoani Tanga.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (kushoto) wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na REA Awamu ya Pili (REA II) iliyokuwa inasomwa na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Tanga Mhandisi Abdulrahman Nyenye (hayupo pichani)
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Tanga Mhandisi
Abdulrahman Nyenye akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini
chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mbele ya Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo pamoja na watendaji wengine kutoka Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Wilaya ya Handeni, Wizara ya Nishati na Madini, TANESCO na
wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela akielezea mafanikio ya miradi ya
usambazaji wa umeme vijijini iliyotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu
ya Pili (REA II).
Na Greyson Mwase, Tanga
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa serikali
imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 kila mwananchi
anapata umeme wa uhakika na kupelekea uchumi wa nchi kukua kwa kasi.
Profesa Muhongo aliyasema hayo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa
miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati
Vijijini Awamu ya Pili (REA II) kutoka kwa watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) mkoani Tanga. Profesa Muhongo yupo mkoani Tanga kwa ajili ya
kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na REA pamoja na kuzungumza
na wananchi.
Profesa Muhongo alisema kuwa kwa kutambua mchango wa nishati ya umeme
katika ukuaji wa viwanda nchini, serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha kuwa kasi
ya usambazaji wa umeme vijijini inaongezeka ili ifikapo mwaka 2020 mgawo wa
umeme uwe ni historia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...