THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KITUO CHA TIC WATEMBELEA MIRADI MBALIMBALI ILIYOWEZESHWA NA KITUO HICHO.

0001
Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari akisikiliza na kuandika maelezo ya Pastory Mroso Meneja Mkuu wa Mlimani City Group wakati alipotembelea mradi mpya wa ujenzi wa kumbi mpya za mikutano na kujionea maendeleo ya ujenzi huo, Mkurugenzi huyo amefanya ziara hiyo ili kuona maendeleo na shughuli za uwekezaji wa kampuni hiyo nchini hapa nchini ili kutambua changamoto na mafanikio yaliyopo katika uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini, waliosimama nyima kutoka kushoto ni Pendo Gondwe Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC , Phina Lyimo Meneja Uhamasishaji na Uwekezaji TIC na Veronica Mrema Afisa Uhamasishaji na Uwekezaji TIC.
0002
Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa kituo hicho kutoka kulia ni Phina Lyimo Meneja Uhamasishaji na Uwekezaji TIC na Veronica Mrema Afisa Uhamasishaji na Uwekezaji TIC na Pendo Gondwe Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC wakati Kaimu Mkurugenzi huyo alipotembelea ujenzi wa kumbi mpya za Mlimani City.
4
Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari akionyeshwa picha ya kumbi mpya za Mlimani City zinazoendelea kujengwa hazipo pichani na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mlimani City Group Pastory Mroso wakati alipotembelea mradi huo ili kuona maendeleo ya uwekezaji wa kampuni hiyo nchini.
001
Meneja Bidhaa Mwandamizi wa Kampuni ya Super Doll .inayotengeneza matela ya maroli iliyo chini ya kampuni mama ya Super Star Group Bw. Ibrahim Juma akiwaelezea wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wakati walipoitembelea kampuni hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ili kuona tija na changamoto za uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini, Ziara hiyo iliandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC.