Klabu ya Simba inayo furaha kubwa sana kuwaarifu kuwa imeshakamilisha maandalizi yote ya mechi ya kesho dhidi ya timu ya AFC Leopards ya nchini Kenya, Mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa uliopo Dar es salaam

Mechi hiyo ya kimataifa itatanguliwa na burudani mbali mbali za muziki zitakazoongozwa na bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta pamoja na wasanii wa muziki wa kizazi kipya.

Mbali ya burudani hizo.pia kutakuwa na shamra shamra nyingine.zitakazonegesha kilele cha wiki ya sherehe zetu zinazojulikana kwa umaarufu wa Simba Day.

Klabu pia itatumia mechi ya kesho kuwatambulisha wachezaji wote watakaotumika kwenye msimu ujao wa ligi 2016|17.wakiwemo wale wapya waliosajiliwa msimu huu.

Sanjari na hayo kesho tutazindua rasmi jezi mpya za msimu na pia zitaanza kuuzwa pale uwanjani Taifa kwa thamani ya shilingi elfu ishirini kwa jezi moja.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ataongoza viongozi mbali mbali wa kitaifa kwenye sherehe hizo muhimu ambazo pia ni maadhimisho ya miaka themanini toka kuanzishwa kwa klabu yetu.

Kiingilio kwenye mechi hiyo ni shilingi 5,000 kwa mzunguko.10,000 kwa viti vya orange.15, 000 kwa VIP C. 20, 000 kwa viti vya VIP B na shilingi 25, 000 kwa VIP A.

Tunawaomba sana watu watakaokuja uwanjani kesho wajihadhari na matukio yote yatakayoashiria uvunjifu wa amani.ili kutoa fursa kwa watu kupata burudani na kuona kwa raha mchezo huu muhimu ambao ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom na kombe la Shirikisho.

Imetolewa na 
HAJI S.MANARA
MKUU WA HABARI
SIMBA SC

SIMBA NGUVU MOJA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...