Na mwandishi wetu, Berlin
Nilipata kusoma habari moja kutoka katika moja ya Vitabu vya Mwalimu Nyerere kuwa, Kijana anayetumia pesa na Chakula cha Kijiji,akitumwa ughaibuni kutafuta kilicho chema,kisha akapotelea huko asirejeshe chochote Nyumbani kwao,huyo atakua amefanya Uhaini.Tunataka Vijana wanaokwenda Ughaibuni na kuleta Chakula Nyumbani.
Nimelazimika kuyakumbuka maneno haya baada ya kuona na kuskia habari za Petro Itozya Magoti (pichani) Kijana wa Kitanzania aliyeko Ulaya(hususani ktk Nchi ya Ujerumani) akihudhuria Mafunzo ya Uongozi na Mahusiano ya Siasa za Kimataifa.

Petro Magoti amepata fursa ya kipekee ya kuwa Mwakilishi wa Tanzania ktk Mafunzo hayo yanayohusisha Nchi 27 DUNIANI na ktk Bara la Afrika  wametoka Vijana 14 pekee na kati ya hao Tanzania wamechaguliwa Vijana 2, kwa bahati mbaya kijana mmoja hakuweza kuhudhuria kutokana na Majukumu aliyo nayo kwa sasa. Mafunzo hayo ni ya siku 60,tangu Augst 4, hadi Octoba 4 mwaka huu.
Msingi mkubwa wa Mafunzo hayo ni kuwaandaa Vijana katika Misingi ya Uongozi,pamoja na kujadili namna ya kutumia Fursa zilizopo ktk Nchi husika ili kuwawezesha zaidi kujiendeleza ktk Mahusiano ya Kitaifa na Kimataifa,kuwa na uwezo mahsusi wa kuzitumia Fursa zilizopo kwa Maendeleo ya Nchi zao.
Imepangwa mafunzo hayo yafanyike ktk Majiji Makubwa manne Nchini Ujerumani ambayo ni Berlin City, Humburge, Hannover na Munster, kisha Uholanzi ktk Majuma mawili ya Mwisho.
Hii ni Fursa ya kipekee kabisa kwa Vijana wa Afrika na hasahasa Tanzania kwani kupitia nafasi hiyo,licha ya kujifunza zaidi, Tanzania tutakua Mwakilishi wa kuitangaza Nchi yetu katika maswala ya Uchumi,Siasa na maswala ya Kijamii.
Kupitia Utangamano huo(Intergration) Tanzania inajipambanua zaidi katika Fursa zake za Kibiashara na Kitalii. Hivyo ni Matarajio yetu kuwa baada ya ukamilifu wa Mafunzo hayo kutafuatiwa faida kubwa zaidi za kiuchumi ktk Nchi yetu kutokana na uwekezaji. Kusoma zaidi BOFYA HAPA



Mdau Petro Magoti akimkabidhi Bendera Profesa  Reinhold Hemker ambaye ni Mbunge mstaafu wa Bunge la Ujerumani  wa Chama cha SPD kama  ishara ya Kushirikiana na CCM mahusiano ya Kimataifa
 Mdau Petro Magoti Akiagana na Professor Karl Heiz Knoop ambaye ni mmiliki mashuhuri wa viwanda sehemummbalimbali Duniani baada ya Kufungua Mafunzo ya Uongozi. Kushoto ni  Meya wa Mji wa  Bugermeister Bw. David Osthotlhoff 



 Mdau Petro Magoti Akiwa na Mama Hemker Castin (kushoto) na mke wa Professor Knoop Muda Mfupi ya Kumaliza Kuongelea TANZANIA kwa Umuhimu wao kuja Kujenga Viwanda vya Vifaa vya Kilimo.
Mdau Petro Magoti akiwa na Wazee waasisi  wa Chama cha SPD waliopigana Vita vya pili  vya dunia dunia dhidi ya Urusi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...