Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akizungumza na waandishi kukemea hatua ya kuahirishwa Baraza la Madiwani leo kwasababu za kutotimia akidi. |
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro (pichani juu) amekemea kitendo cha kuahirishwa kikao cha Baraza la Madiwani katika
jiji la Arusha kuwa kinawanyima wananchi haki ya kuwakilishwa katika
baraza hilo linalojadili maendeleo.
Kikao hicho kimeshindwa kufanyika baada
ya madiwani 14 pekee kuhudhuria katika ya madiwani 36 ambao ni wajumbe
halali wa kikao hicho.
Meya wa Jiji hilo Mstahiki Kalist Lazaro amesema
amelazimika kuahirisha kikao hicho baada ya akidi kushindwa kutimia huku
akidai baadhi ya madiwani wamejificha wakiogopa kukamatwa na polisi kwa
kuhamasisha maandamano ya Septemba Mosi.
Mkuu wa wilaya amepinga kauli hiyo ya
Meya na kusema akiwa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
amewasiliana na Mkuu wa polisi wa wilaya(OCD)ambaye alikanusha taarifa
za kutafutwa madiwani hao.
Aliwataka madiwani hao watimize wajibu
wao wa kuwawakilisha wananchi waliowachagua badala ya kutoa sababu
zisizo na mashiko huku wakifahamu vikao vya baraza la madiwani vipo
kisheria na vina gharama kuviandaa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...