THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MHE. GEORGE MASAJU AVIASA VYAMA VYA SIASA KUHESHIMU KATIBA YA NCHI “Napenda kuvishauri vyama vya siasa nchini kuacha kutumia kauli za kibabe na vitisho kwa kisingizio cha kutumia haki zao za kikatiba, hali hiyo itapelekea vyombo vya dola kuchukua hatua kwani ni viashiria vya uvunjifu wa amani”. Amesema Mh.Masaju.
 Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju alipokuwa akizungumza nao masuala mbalimbali yaliyohusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,alipokuwa akizungumza mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar leo.

 Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju akifafanua masuala mbalimbali kuhusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,alipokuwa akizungumza mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar leo.PICHA NA MICHUZI JR

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar leo,Masaju amesema kuwa polisi wamesema kuwa wana hali ya kuzuia mikutano na maandamano iwapo watabaini kuwa yataibuka mambo yatakayohatarisha amani ya nchi,Masaju amesema kuwa maandamano hayo yataleta madhara na athari kama maandamano hayo ya UKUTA-Septemba mosi mwaka huu.

Amesema kuwa madhara na athari ya maandamano hayo ni kubwa kutokana na siku hiyo itakuwa mahsusi kwa ajili ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwao,akaonngeza kuwa siku hiyo kutakuwa na tukio muhimu la kupatwa kwa Jua huko Lujewa mkoani Mbeya ambapo ni muhimu kwa nchi kupata manufaa kwa Watalii kuja kwa wingi na kuweza kunufaika Kiuchumi. 

Masaju amesema kuwa vyama vya siasa nchini vinatakiwa kutumia vyema haki zao za msingi zilizoanishwa katika katiba badala ya kutumia, nguvu, ubabe na kupelekea kutishia hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.

Masaju amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya wanasiasa wanaotoa vitisho vya kuitisha mikutano kinyume na taratibu za kisheria kwa kisingizio cha haki za kikatiba jambo ambalo sio kweli.“Napenda kuvishauri vyama vya siasa nchini kuacha kutumia kauli za kibabe na vitisho kwa kisingizio cha kutumia haki zao za kikatiba, hali hiyo itapelekea vyombo vya dola kuchukua hatua kwani ni viashiria vya uvunjifu wa amani”.

Masaju aliwataka Wanasiasa kuwa wakweli na kuacha kuwapotosha wananchi kuwa wananyimwa haki ya kufanya mikutano kwani wapo baadhi yao wanaofanya mikutano katika majimbo yao baada ya Jeshi la Polisi kujidhirisha kwamba kutakuwa na hali ya amani na utulivu”. Alisema Mhe. Masaju.

Aidha Masaju alipongeza juhudi zinazofanywa na viongozi mbalimbali wa dini nchini kwa jitihada wanazofanya za kushauri katika kufika muafaka wa hali ya kisiasa nchini na kuwashauri kuhubiri amani na utulivu kwa waumini wao. 

Akitoa ufafanuzi wa tamko la baadhi ya vyama vya upinzani kutaka serikali kuvifuta vyama hivyo Mhe. Masaju alisema kuwa suala hilo ni kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu katiba hiyo inaruhusu mfumo wa vyama vingi.


Kuna Maoni 4 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Amani iliyopo inatosha kwa haki zote kupatikana wala hakuna atakayeivunje hata akiandamana mwaka mzima.

 2. Anonymous Anasema:

  Mbona mikutano ya siasa imekuwepo tangu 1992 lakini amani haikuvunjika wala watu hawakuacha kazi?

 3. Anonymous Anasema:

  Inasikitisha kupoteza askari kwa mauwaji.

  Lakini polisi wengi hudhulumu wananchi, hata raisi alitoa hotuba kuwa kuna kesi za kubambikizwa, raia wamechoka, ndo maana jambazi wauwaji waovu wanaonekana kwa wananchi kadhaa kama wanawasadia kisasi. japo nakubali muono huo ni mbaya na mwovu. Lakini polisi wafate ushauri wa raisi.

 4. Anonymous Anasema:

  Rais alizuia mikutano ya kisiasa kwanza kabla ya ukuta na kabla ya zuio la polisi kuzuia ukuta.

  Rais hakuzuia mikutano kwa kukemea ukuta. Ni miongoni mwa mbinu zake za kutekeleza "kauli mbiu" yake ya hapa kazi tu. Ili watu wafanye kazi tu.

  Naona Mh mwanasheria umeteleza kidogo hapo uliposema katazo la polisi ni baada ya kupewa habari na polisi kuhusu uvunjifu wa amani. Raia wakiona uongo unafanya waone chadema nafuu. Uko upande wa sheria basi sema kweli, usidhani ukisema ukweli utatumbuliwa. Ukimtetea raisi kwa uongo anaweza kukutumbua yule, hapendi uongo.