Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) kilipata fursa ya kutembelewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe kwenye maonesho yanayoendelea ya wakulima NaneNane Kitaifa katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Akiwa kwenye banda la AICC Mhe.Mhandisi Kamwelwe aliweza kupata taarifa juu ya shughuli na huduma zinazotolewa na Shirika hili la Umma ambalo limesimama imara toka kuanzishwa kwake mwaka 1978. Pamoja na kupongeza utendaji mzuri wa Kituo katika shughuli za utalii wa mikutano, alisisitiza umuhimu wa AICC kuendelea kutangaza vivutio vilivyopo Tanzania.

Mbali na kushiriki kwenye maonesho ya NaneNane, AICC pia ilipata mualiko wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi, Bw.Jomaary M. Saturi kwenye hafla fupi ya kuelezea fursa za uwekezaji zinazotarajiwa kufanyika Mkoa wa Lindi kutokana na ugunduzi wa gesi na viwanda vinavyotarajia kujengwa.

Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo ambapo alitoa wito kwa AICC kuwekeza katika sekta ya utalii wa mikutano kwa kujenga Kituo cha Mikutano cha kisasa Mkoa wa Lindi kwa kuwa hakuna kabisa kumbi za kisasa zitakazoweza kukidhi mahitaji yatokanayo na uwekezaji mkubwa unaotarajiwa.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mh. Isack Kamwelwe akisisitiza jambo wakati alipotembelea banda la AICC, Maafisa wa AICC na JNICC wakimsikiliza kwa makini.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Mhandisi Isack Kamwelwe akiweka saini kitabu cha wageni alipotembelea banda la AICC kwenye maonesho ya NaneNane Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.Godfrey Zambi akizungumza wakati wa kikao na wadau mbalimbali kwenye wa hafla ya uwekezaji iliyofanyika ukumbi wa Andrew Kagwa, Lindi.
Maafisa kutoka AICC wakisikiliza kwa makini wakati wa hafla ya uwasilishaji wa fursa za uwekezaji zinazopatikana Mkoa wa Lindi. Kutoka kulia ni Afisa Mkuu Masoko na Utafiti wa AICC Bi.Linda Nyanda na Afisa Itifaki na Uhusiano wa JNICC Bi.Beatha Hyera.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...